Omega 3 humsaidia mtoto kukuza ubongo, kutengeneza retina
kwenye mboni ya macho, na kutengeneza nervous system.
Omega 3 humsaidia mama kuzuia preeclampsia na postpartum
depression.
Njia kuu mtoto kupata Omega 3 ni kutokana na vyakula
anavyokula mama. Kama mama atashindwa kupata vyakula vya kutosha vyenye Omega 3
basi mtoto atachukua Omega 3 iliyoko mwilini mwa mama ambayo mara nyingi iko
kwenye ubongo wa mama.
Basi iwapo mama hatapata Omega 3 ya kutosha anaongeza risk
ya kupata Pospartum depression, mtoto mwenye uzito mdogo, preterm
labor(mtoto kuzaliwa kabla ya muda), au csection(kuzaa kwa upasuaji).
Watoto ambao wamepata Omega 3 ya kutosha wameonyesha kuwa na
attention spans kubwa na upeo mzuri kuliko watoto wengine. Pia walikuwa mbele
zaidi katika ukuaji.
Kwa watoto hupunguza matatizo ya kitabia, na kwa watu wazima
hupunguza chance za kupata kansa ya maziwa na prostate.
Hata kama wewe si mjamzito ni vizuri kupata Omega 3 ya
kutosha kupitia mlo wa kila siku.
Wakati wa ujauzito unashauriwa kupata angalau
250mg kila siku na katika trimester ya mwisho( miezi mitatu ya mwisho)
kwasababu katika kipindi hiki mtoto hutumia asilimia 70 ya Omega 3 kujenga
ubongo wake na nervous system yake.
Vyanzo vya Omega 3 katika Vyakula:
Omega 3 inapatikana katika samaki na mafuta ya samaki hasa
hasa samaki wenye mafuta mengi kama vibua(mackerel), herring, salmon, dagaa,
tuna.
Vyakula Vyenye Omega 3 |
Lakini ni vizuri pia kujua kwamba samaki wengi siku hizi wamekuwa
na sumu ya mercury kwasababu ya machafuko ya kimizingira hivyo unaweza pia
ukapata Omega 3 kutoka kwenye mayai, mkate, juice, mboga za majani, canola,
sunglower, flaxeed oils na walnuts.
Na kama utapenda kunywa vidonge vya Omega 3 uhakikishe
kwamba havijatengenezwa na maini ya samaki kwani hizi zina asilimia kubwa ya
retinol Vitamin A, ambayo imegundulika kusababisha madhara kwa watoto.
Omega 3
iliyotengenezwa kutoka kwa nyama ya samaki na sio maini ni bora zaidi. Kama
huna uhakika ni bora kununa vidonge maalum vya Omega 3 vilivyotengenezwa kwa
ajili ya wamama wajawazito.
Je, Ni aina gani ya samaki ambao wana madini ya zebaki? Mama mjamzito anatakiwa ale samaki wapi ili asipate madhara?
ReplyDeleteDagaa wakubwa na papa
DeleteNikiwa mjamzito naweza kufunga kula chakula masaa 24?
ReplyDelete