Thursday, June 21, 2012

Mazoezi kwa mama mjamzito wiki ya Nane

Kwa wale mlioniuliza jinsi ya kupangilia mazoezi maalum kwa mama mjamzito katika siku yako, nitakuwa natoa ratiba ya mazoezi kila wiki. Kwa maelezo zaidi ya kila zoezi angalia katika maada zilizopita. 
 
Maelezo ya jinsi ya kuyafanya haya mazoezi na umuhimu wake pamoja na ratiba ya mazoezi kwa wiki zilizopita:

Hii ratiba ni ya wiki ya nane kama wewe ndio kwanza unaanza, rudi katika maada zilizopita na anza kwa kufanya mazoezi ya wiki zilizopita. Nitawapa ratiba nyingine wiki ijayo kuongeza challenge kidogo katika mazoezi.

Pamoja na mazoezi ni vizuri pia uzingatie lishe bora kwa afya yako na mtoto kama tulivyoongelea katika maada za nyuma. 

Mazoezi kwa mama Mjamzito Wiki ya Nane:

Monday, June 11, 2012

Stage ya kwanza ya labor


Kuna stage tatu ambazo mwanamke ambaye anajitayarisha kujifungua anapitia wakati wa labor.

Hizi ni:
  • Stage ya kwanza ya Labor (Dalili za kuingia labor na mwanzo wa maumivu na kupanuka kwa njia ya uzazi)
  • Stage ya Mpito/Transition (Kuvuka kwa stage ya kwanza kwenda kwenye stage ya Pili)
  • Stage ya Pili ya Labor (Kusukuma mtoto na Kutoa placenta)

Katika maada ya leo tutaongelea dalili za kuanza kwa labor na ni vitu gani vitatokea katika stage hii ya kwanza.

Kabla ya kuanza kwa labor kuna vitu fulani vitatokea mwilini ili kumtayarisha mama na mtoto kwa labor halisi.

Hivi ni pamoja na kupata
  • Braxton Hicks contractions – huku ni kubana na kuachia kwa misuli ya uterus ili kumsukuma mtoto chini. Tofauti na contractions za kweli za labor hizi huja na kuacha na huwa hazina ratiba maalum. Huwa zinaanza kutokea miezi mitatu ya mwisho wa ujauzito.
  • Kuongezeka kwa damu mwilini.
  • Kutoka kwa hormone za relaxin na hyaluronidase – Hormone hizi husaidia kulegeza misuli ya chini ya tumbo na hips ili kuongeza njia ya uzazi.
  • Kutengenezwa kwa Colostrum – maziwa ya mwanzo yenye virutubisho na kinga maalum kwa ajili ya mtoto atakayezaliwa.
  • Kulainika kwa cervix – cervix ni ufunguo au njia ya uterus. Wakati wa ujauzito njia hii inazibwa na utepe mzito ”mucous plug” ili kuzuia vijidudu kumfikia mtoto na pia kuziba njia ya uzazi wakati wa ukuaji wa mtoto.

  • Kutoka kwa utepe wa mucous plug kwenye cervix – Moja wapo ya dalili za kuanza kwa labor ni kutoka kwa utepe wa mucous plug ukeni. Utepe wa mucous plug unaweza kutoka na damu kidogo.

Jinsi mwili unavyofanya kazi wakati wa Stage ya Kwanza ya Labor

  • Kuanza kwa conractions – Kubana na kuachia kwa misuli ya uterus na kusukumwa kwa mtoto. Misukumo hii huambatana na maumivu makali sehemu ya chini ya tumbo ambayo itaendelea kwa ratiba maalum.
  •  Mama Kusikia njaa.
  •  Mama Kusikia kiuu.
  • Mama anaweza kupatwa na tumbo la kuharisha.
  • Dilation – Kufunguka kwa cervix ikiambatana na kutokwa kwa utepe wa ”mucous plug”. Kufunguka huku hupimwa kwa centimeter kidole kimoja kikiwa kama centimeter moja (1). Cervix itafunguka kwa centimeter moja kwa kila saa ya labor kwa kawaida lakini hutofautiana mwanamke kwa mwanamke. 0 cm mpaka 4 cm hutokea wakati wa stage ya kwanza ya labor. 4 -7 cm hutokea lavor inapochangamka na kuwa ngumu. 7-10 hutokea wakati wa stage ya mwisho wakati mwanamke anajitayarisha kusukuma. Centimeter 10 ni sawa na ukubwa wa kichwa cha mtoto na wakati huu ndio mtoto anakuwa tayari kuzaliwa.
  • Effacement – Kutanuka kwa cervix ili kuongeza njia na upana wa cervix ili kusaidia mtoto kupita. Kabla na wakati wa ujauzito cervix ya mwanamke ni pana na ndefu inchi moja au mbili. Wakati wa stage ya kwanza ya labor cervix itaanza kuwa fupi na kupanuka kitendo kinachoitwa effacement au kuiva kwa cervix. Inaweza kuchukua wiki kadhaa mpaka cervix kufunguka kabisa. Effacement hupimwa kwa asilimia. 0% maana yake effacement bado haijatokea na cervix bado haijafunguka. 50% maana yake effacement imefunguka nusu. 100% maana yake cervic imefunguka kabisa.
  • Kama ni mtoto wa kwanza kwa mama, kitendo kitakachotokea kwanza ni effacement ikifuatiwa na dilation. Kama mama kashazaa basi itaanza na kitendo cha dilation kufuatiwa na effacement.
  • Station – Hii ni jinsi gani mtoto ameshuka kwenye njia ya uzazi. Kama mtoto yuko juu ya mifupa basi ni mwanzo wa labor mtoto akishuka chini ya mifupa basi ni karibu na wakati wa kuzaliwa. Hii hupimwa kuanzia -3 , 0 , 3. Ikiwa  -3 kuonyesha kuwa mtoto yupo juu na 3 kuonyesha kuwa mtoto kashuka chini.
 
    
  •  Kutokwa kwa damu – hii ni mojawapo ya dalili ya kuwa cervix inafunguka na kuwa ni mwanzo wa labor. Damu hii itakuwa rangi ya pink au brown.
Kwa wakati huu mama hashauriwi kulalia mgongo kwani kulalia mgongo kutasababisha uterus kushuka mbele wakati wa contractions na kufanya maumivu yawe makali zaidi.

Tumeongelea dalili za kuanza kwa stage ya kwanza ya labor sasa tutaongelea jinsi mwili unavyofanya kazi wakati wa stage ya kwanza na kujitayarisha kuingia stage ya pili.

  • Msukumo wa contraction kuwa na nguvu na maumivu makali zaidi.
  • Kuendelea kuwa na kiuu.
  • Kuondokewa kwa aibu.
  • Kupungukiwa kwa hamu ya kula.
  • Kutaka kwenda haja ndogo mara kwa mara.
  • Kuendelea kwa dilation na effacement.
Kuna uwezekano wa contractions kundelea lakini kufunguka kwa cervix(dilation kusimama) hii husababishwa na:
  • Maumbile
  • Kulainika kwa misuli na mifupa
  • Kuongezeka kwa hormone mwilini
  • Kutengenezwa kwa kinga kwa ajili ya mtoto
  • Baadhi ya misuli ya mwili kupumzishwa
  • Kila mwanamke yuko tofauti kwa hiyo masaa ya kuwa katika stage hii ya labor hutofautiana.Hivyo mama asife moyo kama labor itasimama kwa muda.


Dalili nyingine ya kuwa mama ameingia katika stage ya mwanzo wa stage ya kwanza ya labor:
  • Mwanamke anaweza kuwa na furaha ya kuwa siku imefika lakini kutokuwa na uhakika kama labor imeanza kiukweli ukweli.
  • Mwanamke kutoweza kutulia sehemu moja, kutembea tembea, kuongea sana, kufanya shughuli kama kusafisha nyumba.
  •  Contractions zitapishana kwa dakika 10 au chini ya dakika 10 na kuendelea kwa sekunde 45 -60 na kuongezeka kwa nguvu na kukaribiana zaidi.
  • Contractions kuwa na maumivu makali sana ifikapo sekunde ya 30. Kusikia pressure na maumivu kwenye sehemu ya chini ya tumbo. Kutembea na kuwa busy kutasaidia kwa wakati huu. Mwanamke anaweza kuona mabadiliko mengi kwenye mwili wake kwa wakati huu.
  • Mwanamke ajitahidi kula kunywa maji na kupumzika iwezekanapo ili kutunza nguvu atakayoihitaji hapo baadaye.
  • Kutembea kutasaidia kufungua njia ya uzazi. Kama labor ikisimama usivunjike moyo. Endelea kupata chakula na kupumzika hiki ni kitu cha kawaida.
 Dalili za kuwa mwanamke sasa yuko katika stage ya kwanza ya labor. 
  • Mwanamke kugundua kuwa labor inaanza haswa, kuwa na moyo kuwa anauwezo wa kukabiliana na yale yaliyo mbele yake.
  • Atajaribu position mbali mbali kuona ipi yuko comfortable zaidi wakati wa maumivu.
  • Kutembea kwa wakati huu ni muhimu sana.
  • Maumivu yamekuwa makali zaidi lakini mwanamke atapendelea kuendelea na kazi wakati wa kutulia kwa contractions.
  • Anaweza kuwa na njaa kutokana na labor imekuwa ikiendelea kwa muda gani.
  • Anaweza kuendelea kuongea au kufanya shughuli wakati wa maumivu lakini inaanza kuwa vigumu zaidi.
  • Mabadiliko ya mwili yanaanza kuwa ya kawaida.
  • Contractions zinaendelea kuwa zenye nguvu na nyingi zaidi. Zitapishana kwa muda wa dakika tano na kuwepo kwa sekunde 60.
  • Kuongezeka kwa pressure kwenye sehemu ya chini ya tumbo na kufunguka kwa sehemu hiyo. Kupatwa na maumivu ya mgongo. Kusikia maumivu kama ya siku za mwezi kwenye tumbo.
  • Kusikia kutanuka kwa eneo la chini ya tumbo.
  • Zoezi la pelvic rocks litasaidia kupunguza maumivu kwa wakati huu.(tulishaongelea jinsi ya kufanya hili zoezi kwenye maada zilizopita)
  • Kwa wakati huu anahitaji kutiwa moyo na upendo kutoka kwa watu karibu kwake.
  • Anahitaji nafasi na upepo na aendelee kutembea.
  • Endelea kuhesabu contractions kuona zinaendelea vipi.
  • Jaribu kutotumia nguvu zako kwa kipindi hiki maana ni vigumu kujua utakuwa kwenye labor kwa kipindi gani. Jaribu kuwa busy au fanya kitu cha kufurahisha ili muda uende kwa kasi.
Dalili za kuishia kwa stage ya kwanza ya labor.
  •  Mwanamke kuanza kuingiwa na uoga pale maumivu na contractions zinapozidi.
  •  Mwanamke kutotaka kusumbuliwa na kuwa serious zaidi.
  •  Kuondokewa na aibu
  •  Aendelee kutembea lakini atembee kwa taratibu zaidi.
  •  Anaweza kutaka kupumzika.
  •  Kufumba macho na kusikilizia maumivu.
  • Anaweza kupenda kukaa kwenye choo.
  • Njaa kuondoka.
  • Kutotaka kuongea tena.
  • Kutokwa na jasho .
  • Kutokwa kwa maji ya uzazi.
  • Contractions kuwa kali zaidi kutokuwa na muda wa kupumzika au kupishana kwa maumivu haya. Kuendelea kwa sekunde 60 au zaidi. Kuweka pressure kwenye mfuko wa mkojo na kutaka kwenda haja mara kwa mara.
  • Kazi inakuwa ngumu zaidi, Maumivu makali zaidi mwanamke ajaribu kuwa relaxed kwa kipindi hiki. Kwa sababu kuwa na wasi wasi au uoga kwa wakati huu kutazidisha maumivu zaidi. Pressure kuwa kali zaidi kwenye sehemu ya chini ya tumbo.
  • Ikiwezekana mama akae kwenye sehemu yenye giza au kuzimwa kwa taa
  •  Mama aendelee kutembea tembea na kutokulala au kukaa sehemu moja.
  • Watu wasiweke pressure kwa mama kwa wakati huu
  • Ajitahidi kunywa maji na kwenda chooni mara kwa mara
  • Mama aendelee kuwa na subira katika kipindi hiki na kujaribu kurelax kwasababu labor hutofautiana na huweza kuchukua muda mrefu au kuwa fupi.
 Kama huna uhakika kama labor imeanza au la ni vizuri:
  • Kupumzika au pata usingizi
  • Kunywa maji ya kutosha
  • Kutembea
  • Kuoga

Dalili ya kuwa labor yako inaenda pole pole
  • Contractions zinaanza na kusimama
  • Contractions zinapishana kwa dakika 10 hadi 20
  • Contractions hazikaribiani
  • Contractions hazichukui muda mrefu
  • Contractions haziongezeki kwa ukali au maumivu

Dalili ya kuwa labor yako inaendelea kwa mwendo wa kawaida
  • Contractions zinaenda kwa mwendo wa kawaida
  • Contractions zinapishana kwa chini ya dakika 10 au dakika 10
  • Contractions zinaendelea kwa sekunde 60
  • Contractions zinakaribiana, zinakaa kwa muda mrefu zaidi na zinakuwa kali zaidi jinsi saa zinavyoenda
Dalili ya kuwa labor yako itakuwa fupi sana
  • Contractions zinaanza kwa kukaribiana
  • Contractions zinaanza kwa kuchuku muda mrefu au kuwa ndefu
  • Contractions zinakuwa kali sana
  • Dalili zako zinaanza moja kwa moja bila stage ya mwanzo ya kwanza ya labor.


Mara nyingi wauguzi watafanya uchunguzi kuona jinsi labor inaendelea. Katika uchunguzi huu watatumia mikono au vidole kupima  dilation, effacement, station na jinsi mtoto alivyokaa tumboni.

Kama ikiwezekana ni vizuri kuepukana na vipimo hivi kwasababu vinaweza kusababisha kuchanika kwa mfuko wa uzazi kabla ya muda wake(premature rapture of membranes), kusababisha infection na vijidudu kuingia kwa mtoto, vipimo hivi vitampa mama maumivu ya zaidi, wakati mwingine vipimo hivi si sahihi, na huweza kuongeza risk ya kufanyiwa operesheni.

Kama maji ya uzazi yameshamwagika si vizuri kufanyiwa vipimo hivi.

Katika maada zijazo nitaendelea kuongelea stage ya pili ya labor na position mbali mbali za kusukuma, dawa mbali mbali zinazoweza kutumiwa wakati wa labor na madhara yake, Vitu gani vinaweza kutokea ambavyo vinahitaji umakini zaidi na kuweza kusababisha operesheni,vitu gani vitatokea wakati wa operesheni, ni vitu gani natural mama anaweza kufanya kwa wakati huu aidha kuharakisha labor au kuanzisha labor iwapo inachelewa, kazi ya baba au watu wa karibu kwa mama wakati wa labor.

Saturday, June 2, 2012

Kujisikia Kichefu chefu na Kutapika wakati wa ujauzito (Morning Sickness)


Nusu ya wanawake wote wajawazito hupatwa na tatizo la kujisikia kichefu chefu na kutapika; ni mojawapo ya dalili kuu za ujauzito. 

Husababishwa na kuongezeka kwa hormone mwilini, mara nyingi huanza katika wiki ya sita ya ujauzito na huweza kutokea muda wowote wa siku. 

Madaktari wengine huwa wanaamini ya kuwa ni dalili nzuri kwani humaanisha ya kuwa placenta inafanya kazi vizuri.

Kwa wanawake wengine tatizo hili huisha katika wiki ya kumi na mbili ya ujauzito. Lakini kwa wengine huweza kuendelea kwa kipindi kizima cha ujauzito.

Mara nyingi ni kitu cha kawaida ambacho kinakuja na kuondoka lakini pale ambapo mama anatapika kupita kiasi mpaka anashindwa kubakisha chakula au maji mwilini basi anahitaji kumuona daktari.


Vitu vya kufanya kusaidia au kupunguza tatizo hili:

  1.  Kula milo mingi midogo mara kwa mara badala ya kula milo mikuu mitatu kwa siku. Hii itasaidia kwasababu wakati mwingine tatizo hili linasababishwa na kutokuwa na sukari ya kutosha kwenye damu(low blood pressure). Sukari hii ndio chanzo cha nguvu mwilini. Ukila mara kwa mara chakula kitapokelewa mwilini na kutengenezwa sukari na mwili kuwa na nguvu ya kutosha. 
  2. Kunywa vinywaji nusu saa kabla au baada ya chakula. Usinywe vinywaji na kula chakula kwa wakati mmoja.
  3. Kula mkate wa kukausha(toast au crackers) au matunda yaliyokaushwa dakika 15 kabla ya kumka asubuhi.
  4. Kunwya maji mara kwa mara ili kuzuia mwili kuishiwa na maji (dehydradtion). Jaribu kunywa litre 2.5 kwa siku ikiwa pamoja na maji, chai au juice natural zisizo na sukari ya kuongeza.
  5. Jitahidi usile au kupita sehemu zenye harufu ya chakula zinazozidisha tatizo hili.
  6. Pumzika vya kutosha na pata usingizi wa mchana.
  7. Usikae sehemu zenye joto jaribu kukaa ndani kwenye feni au ac au nje sehemu zenye upepo. Kwasababu joto huzidisha tatizo hili. Pia usiende sehemu zenye watu wengi.
  8. Ndimu, tangawizi zinasaidia, pia unaweza kunywa maji ya ndimu au kula tunda la tikiti maji (watermelon) kupunguza kichefu chefu.
  9. Kula viazi vya  kukausha na chumvi.
  10. Fanya mazoezi.
  11. Usilale baada ya mlo
  12. Usiache kula
  13. Usile au kupika vyakula vyenye pili pili (spicy) au mafuta mengi.
  14. Usinywe kahawa au vinywaji vikali
  15. Kula vyakula vya protein kabla ya kwenda kulala usiku
  16. Fungua madirisha au Tembea nje ili kupata upepo na oxygen ya kutosha.
  17. Weka kijiko kimoja cha maji ya Apple Cider Vinegar kwenye 8 ounces ya maji ya uvuguvugu kisha kunywa asubuhi kabla ya kuamka.

Maji ya Apple Cider Vinegar

18. Kunywa chai za Rasberry leaf, Spear mint/ pepper mint, Anise seed, Fennel seed kabla ya kuamka asubuhi.
chai ya raspberry leaf
chai ya anise seed

chai ya fennel seed


Umwone daktari kama:

Unatapika kupita kiasi mpaka unashindwa kubakisha chakula au maji tumboni au kama kutapika kunaambatana na homa au maumivu.