Wednesday, March 21, 2012

Tatizo la kutokwa na damu katika ufizi wakati wa ujauzito

Kuna wanawake wengine wakiwa wajawazito wanapatwa na hili tatizo la kutokwa na damu katika fizi, kuvimba kwa fizi au kuumwa kwa fizi. 

Hali hii ni ya kawaida kwa kuwa wakati wa ujauzito na hutokana na membrane za mucous mwilini kuwa sensitive sana, kuongezeka kwa mzunguko wa damu kwenye maeneo ya mdomo, na pia kuongezeka kwa hormone ya uzazi ya progesterone ambayo inaweza kusababisha fizi kuwa sensitive zaidi.

Kutatua tatizo hili unaweza ukamtembelea daktari wa meno kusaidia katika kusafisha meno vizuri. Pia jaribu kuongeza vyakula vyenye Vitamin  C katika diet yako kama matunda jamii ya machungwa. Piga mswaki mara mbili kwa siku, tafuta mswaki laini ili usiumize fizi wakati wa kupiga mswaki.

Pia jaribu kupunguza kula vitu vyenye sukari nyingi kama pipi, soda n.k Pia kama unatatizo la kusikia kichefu chefu na kutapika kwa wakati huu jaribu kupiga mswaki kila mara unapotapika ili kuzuia bacteria mdomoni.No comments:

Post a Comment