Iron inatumika
kutengeneza hemoglobin, protein inaytomika katikca red blood cells kubeba
oxygen kwenda kwenye viungo mbali mbali vya mwili. Kama mama mjamzito unahitaji
damu ya kutosha kwa mama na mtoto. Iron ni muhimu kuhakikisha wewe na mtoto
mnapata damu ya kutosha kwa wakati huu.
Usipopata
Iron ya kutosha mwili wako utamaliza Iron iliyoko mwilini hali itakayosabibisha
kupata anaemia.
Kama
ukipata anaemia katika trimester mbili za mwanzo wa ujauzito kuna uwezekano wa
mtoto kuzaliwa mapema kabla ya muda wake yaani preterm na kuwa na uzito mdogo
kupita kiasi.
Mama
mjamzito anahitaji 27mg za Iron kwa siku mara mbili ya mwanamke asiye mjamzito
na utaendelea kuhitaji Iron ya kutosha iwapo unanyonyesha.
Dalili za
upungufu wa Iron kwa mama mjamzito ni pamoja na uchovu, kutoweza kupuma vizuri,
ngozi isiyongaa, na kucha zilizokauka.
Vyakula
vyenye asilimia kubwa ya Iron:
Nyama, samaki, kuku, maharage, na mboga.
Vyakula vyenye Iron |
No comments:
Post a Comment