Thursday, March 15, 2012

Umuhimu wa Protein Kwa Mama Mjamzito


Protein ni muhimu mno kwa ujengaji wa mwili wa mama na wa mtoto. Katika trimester ya pili na tatu(miezi ya tatu ya pili na ya mwisho) mtoto anakuwa kwa kiasi kikubwa sana na ni katika kipindi hiki mama asipopata protein ya kutosha basi mwili utafanya kazi kubwa na kuathirika.

Katika trimester ya kwanza na pili mama anahitaji 60 - 80gms za protein kila siku hii huongezeka mpaka 80 - 100 gms katika trimester ya tatu.

Kuna vyakula vingi sana vyenye protein kwahiyo huwezi kuboreka na kukosa choice ya vyakula. Chini ni mifano ya vyakula vya Protein na kiwango cha Protein ili kukusaidia kujua jinsi ya kutosheleza mahitaji yako ya protein ya kila siku.

Vyakula vyenye asilimia kubwa ya Protein


Mifano ya vyakula vyenye gram 20 ya protein katika makundi mbali mbali.

Maharage, Jamii ya kunde na Karanga
 • 3oz Karanga
 • Kikombe kimoja na nusu cha maharage yaliyopikwa

Maziwa, jamii ya maziwa na mtindi
 • 2/3 kikombe cha cottage cheese
 • Vikombe viwili vya mtindi
 • 3oz ya aina nyingine za cheese/jibini kama swiss, cheddar
 • 2oz cheese aina ya parmesan
 • Mayai matatu
 • Glass mbili na nusu ya maziwa

Nyama na Samaki
 • 3oz, nyama  aina ya kuku, ya ngombe, mbuzi, nguruwe, turkey
 • 3oz samaki aina ya salmon, trout tilapia
 • Shrimp/kamba wakubwa 17 au kikombe kimoja na nusu cha shrimp wadogo
 • 31/2 nyama ya lobster, crab

No comments:

Post a Comment