Mama
mjamzito au anayenyonyesha anahitaji 1600 hadi 2000 mg za calcium kila siku.
Kwa sababu wanawake wengi hawali vyakula bora huwa wanaishia kupata 600mg
kwa siku ambazo hazitoshi. Calcium ni muhimu sana kwa mama na mtoto wakati wa ujauzito
na kunyonyesha.
Kwa mama
calcium inasaidia kuweka blood pressue sawa na kupunguza kupata magonjwa kama
preeclampsia ugonjwa unaoweza kumpata katika miezi ya mwisho ya ujauzito.
Calcium pia inamsaidia mama kuweza kupata usingizi mzuri usiku na kupunguza
kuuma kwa miguu. Hivyo ni vizuri kupata chakula chenye calcium kabla ya kulala.
Kwa mtoto
afya njema inapatikana pale anapopata mg 200 hadi 300 ya calcium kwenye
skeleton yake wakati wa trimester ya tatu. Pia kiwango hicho kinapatikana
kutoka kwenye maziwa ya mama pale atakapozaliwa na kunyonya. Mama akipata
kiwango kinachotakiwa cha calcium itamsaidia mtoto kusawazisha blood pressure
yake pindi atakapozaliwa.
Mwili wa
mama mjamzito unauwezo zaidi wa kuweka calcium kwenye mifupa na mwili kuliko mwanamke asie mjamzito. Hii
ni njia ambayo inamsaidia mwanamke mjamzito kuhimili mahitaji ya mtoto katika
trimester ya tatu na baada ya kujifungua anaponyonyesha. Kama mama ataweza
kupata calcium nyingi wakati wa ujauzito basi hata baadaye akizeeka anaweza
kujikinga na magonjwa ya osteoporosis(kulainika kwa mifupa) ambayo hutokea
katika miaka hiyo.
Magnesium
Magnesium
na Calcium inasaidiana kwa kiasi kikubwa katika kuendesha shughuli mbali mbali
za mwili. Kukosekana kwa Magnesium ya kutosha wakati wa ujauzito kunaweza
kusababisha kupata uchungu kabla ya muda, na kuongezeka kwa matatizo ya nerve
kwa mtoto kama ya cerebral palsy.
Vyakula
vyenye Calcium
Maziwa na
vyakula vyenye jamii ya maziwa kama jibini na mitindi vina Calcium nyingi za
kutosha. Vyakula vingine ni pamoja ufuta, tuna, kale, mustard greens, maharage,
mayai, spinach na whole grains.
Vyakula
vyenye Magnesium
Mboga za
majani yenye rangi za kijani iliyokolea, whole grains, vyakula jamii ya karanga
na njegere. Pia kula vyakula na juisi ya machungwa itakupa vitamin c ambayo
itawezesha mwili kutumia Calcium, Iron na folic acid kwa ufanisi zaidi.
Kuliko
kutumia vitamin supplement za calcium na magnesium ni vizuri mama akijitahidi
kupata hivi virutubisho moja kwa moja kutoka kwenye chakula kwani baadihi ya
madawa yanauwezo kusababisha lead poisoning kama zikitumiwa kwa muda mrefu.
Mama kupata magnesium ya kutosha kutamsaidia mtoto wakati wa labor. Mdundo wa moyo wa mtoto wakati wa labor unakuwa uko sawa na pia kuzuia matatizo mengine kwa mtoto wakati wa labor.
No comments:
Post a Comment