Monday, March 12, 2012

Kiungulia na Gas wakati wa Ujauzito

Kila ujauzito uko tofauti lakini kuna baadhi ya vitu ambavyo wanawake wengi huwa wanaexperience katika ujauzito wao hivi ni pamoja na kiungulia(Heartburn) na kusikia gesi tumboni. Leo tutaongelea jinsi ya kuepukana au kuponya vitu hivi ukiwa katika hali hii. Katika nakala zijazo tutajaribu kugusia matatizo mengine ambayo yako common kwa wamama wajawazito.Kiungulia(Heartburn)

Inaweza kusababishwa na nervous tension, hali ya acidi nyingi katika tumbo,kurelax kwa misuli ya tumbo ambayo itasababisha chakula kurudi juu tumboni, au kwa sababu ya ukuaji wa uterus basi tumbo limesukumwa juu. Hii hali inawakumba wanawake wengi katika nusu ya mwisho wa ujauzito

1. Jaribu kuchunguza ni vyakula gani ukishakula unapatwa na kiungulia. Ukisha vitambua viondoe katika diet yako ya kila siku. Mara nyingi vyakula vyenye mafuta au vyakula vyenye spices nyingi ni tatizo kwa wanawake wengi.

2. Jaribu kufanya mazoezi kidogo ukipatwa na hali hii.

3. Kula mapapai,mananasi, apples au mtindi, maziwa pia mkate uliokaushwa(toast) baada ya mlo. Hivi vyakula vinaweza kusaidia kutuliza kiungulia.

4. Wakati wa kula, jaribu kula chakula katika portion ndogo ndogo badala ya kula mlo mmoja mkubwa kamili. Pia jaribu kula taratibu na tafuna chakula vizuri.

5. Usinywe vinywaji vyenye gas.

6. Jaribu kutembea baada ya mlo.

7.Kula milo midogo mingi mfano kama uko mbali na nyumbani kula karanga au matunda yaliyokaushwa .

8.Usinywe vinywaji wakati wa kula, jaribu kunywa maji mengi kabla au baada ya mlo. Kama lazima unywe wakati wa kula basi kunywa glas ya maji yenye nusu ndimu iliyokamuliwa.

9. Kahawa na sigara zinachangia kwa kuudhi tumbo.

10. Usiwe unalala mara baada ya kula.

11. Chai aina ya "Anise" au "Fennel" baada ya mlo inasaidia tumbo kufanya kazi ya kusaga chakula vizuri.


Matatizo ya Gas

1. Jaribu kuchunguza ni vyakula gani ukishakula vinasababisha gas. Ukisha vitambua viondoe katika diet yako ya kila siku.

2. Lala na jaribu kuvuta pumzi kutoka tumboni.

3. Fanya zoezi la Pelvic Rocking(Zoezi la tatu katika nakala hii "Mazoezi maalum kwa mama mjamzito").

4. Usinywe vinywaji vyenye gas.

No comments:

Post a Comment