Monday, March 12, 2012

Umuhimu wa Folic Acid Kwa Mama Mjamzito

Folic Acid ni jamii ya Vitamin B inayosaidia katika ukuaji na utengenezaji wa cell za mwili ambazo ni muhimu sana katika wiki za mwanzo za ukuaji wa mtoto. 

Inasaidia katika kutengeneza ubongo na uti wa mgongo. Bila ukuaji mzuri wa hivi viungo kuna chance kubwa zaidi ya kupoteza mtoto kwa miscarriage na pia wanaweza wakapata matatizo ya nerve(Neural Tube Disorder)

Haya matatizo yanaweza kujitokeza kama magonjwa ya spina bifida na nancephaly. Matokeo yake ni kwamba mtoto anaweza akaparalzye miguu na kupata magonjwa ya kibofu na haja.

Magonjwa kwa mtoto aliyekosa Folic Acid Ya Kutosha

Umuhimu wa Folic Acid:
  • Utengenezaji mzuri wa cell za mwili.
  • Utengenezaji mzuri wa damu.
  • Kupunguza risk za magonjwa ya moyo na stroke.
  • Husaidia kukinga magonjwa kama cancer, colon cancer na cervical cancer.
  • Hupunguza chance ya kupata magonjwa ya Alzheimers.

Vyakula vyenye Folic Acid:

Mboga nyingi za majani ni vyakula vizuri vyenye Folic Acid, majani ya kunde, maharage, kuku, nyama ya ngombe, uyoga, spinach, lettuce, broccoli, mahindi, maparachichi na juisi ya machungwa, juisi ya nyanya.
Vyakula Vyenye Asilimia kubwa ya Folic Acid


No comments:

Post a Comment