Wednesday, March 28, 2012

Tatizo la kuvimba na kuuma kwa miguu wakati wa ujauzito

Kuuma na kuvimba kwa miguu wakati wa  ujauzito ni tatizo ambalo hujitokeza kwa wanawake wengi. Hili tatizo likitokea hasa hasa miezi ya mwisho wa ujauzito, husababishwa na kutokuwa na calcium na chumvi ya kutosha mwilini, pialinaweza jitokeza kama damu inashindwa kuzunguka vizuri mwilini. 



Jinsi ya kupunguza au kuzuia hili tatizo.
  • Jaribu kufanya mazoezi ya  kutembea, kuogelea kadri ya uwezo wako.Kama tulivyoongelea kwenye mada ya kwanza ya mazoezi.
  • Jaribu kufanya mazoezi ya kunyoosha misuli kama ya Yoga.
  • Jaribu kupata massage ya mwili mzima angalau mara moja kwa mwezi.
  • Fanya mazoezi ya pelvic rocking kusaidia mzunguko mzuri wa damu, chuchumaa mara kwa mara, kaa style ya kihindi/ tailor sitting, lala na miguu ikiwa imeegeshwa juu ya mito. Mazoezi haya yote tulishaiongelea jinsi ya kuifanya kwenye maada ya mazoezi maalum kwa ujauzito pia jinsi ya kulala ili kuhakikisha damu huzunguka vizuri.
  • Hakikisha unapata calicum na chumvi ya kutosha katika diet yako. Kama tulivyoongelea kwenye maaada ya umuhimu wa Calcium kwa mama mjamzito.
  • kama mguu unauma jaribu kusimamia kwenye huo mguu kwa dakika chache.

No comments:

Post a Comment