Kwa ajili ya afya ya mama na mtoto ni muhimu sana mwanamke
apate chakula bora. Ukosekanaji wa chakula bora kunaweza kukasababisha mtoto
kuzaliwa kabla ya mda wake au na uzito mdogo ambao unaweza ukachangia
katika kuzuia ukuaji wa ubongo na mwili.
Kwa mama anaweza akapata anaemia, infection, matatizo katika
placenta, matatizo katika labor, c-section(kuzaa kwa upasuaji wakati wa
kujifungua), kutokupona kwa haraka, matatizo katika kunyonyesha, toxemia na
pre-eclempisa(haya ni magonjwa yanayosababishwa na maini kutoweza kufanya kazi
yake vizuri na mwili kujitahidi kutoa protein kutoka sehemu nyingine za mwili
kwa sababu hamna protein ya kutosha).
Dalili zake ni pamoja na kuwa na protein
kwenye mkojo, blood pressure kuwa juu, kuumwa kwa kichwa, kusikia kizungu
zungu, kuzimia, kuvimba kwa viungo n.k
Mama
mjamzito anatakiwa apate 100 grams za protein kwa siku.
Ifuatayo ni mlo kamili anaotakiwa apate mama mjamzito kila siku ya ujauzito wake kwa
afya bora:
Maziwa na vyakula
vya jamii ya maziwa: Glasi nne au zaidi ya maziwa ya aina yoyote pamoja na/au vyakula vyenye jamii ya maziwa kama jibini, mtindi,siagi, ice cream. Maziwa ni
muhimu kwa protein, calcium, vitamins na virutubisho vingi. Vitasaidia ukuaji
wa mifupa, misuli na nerves. Ni muhimu kwa damu yenye afya, kusaidia usingizi
na kusawazisha mdundo wa moyo.
Mayai:
Mayai mawili kwa siku husaidia kuupa mwili protein, vitamins minerals na vitamin A
ambayo itasaidia kuzuia infections.
Protein:
Serving mbili ya samaki, maini , kuku, nyama ya ngombe, mbuzi, kondoo au
nguruwe, maharagwe au jibini. Kusaidia ujengaji mifupa, meno, misuli, ubongo na
mwili kwa ujumla. Ukosekanaji wa protein ya kutosha kutasababisha kuchoka,
uvimbe na kutojisikia kula au appetite ndogo.
Mboga za
majani: Spinach, cabbage, collard greends, mchicha, matembele. Mboga hizi ziwe
fresh na zile zenye rangi ya kijani iliyokolea(hizi ndio zenye virutubisho vya
kutosha). Mboga hizi zitakupa Vitamin A
na B, pia virutubisho vitakavyosaidia mwili kuabsorb protein ya kutosha,
ukuaji wa mwili, na utengenezaji wa damu. Kutopata mboga za kutosha kunaweza
sababisha mama kupata anemia.
Whole
Grains: Vipande vinne vya Mkate wa whole grain, mkate wa mahindi, vitaupa mwili
vitamin B na carbohydrate kwa ukuaji wa misuli na nerves.
Vyakula
vyenye vitamin C: Kipande kimoja au viwili vya machungwa au juisi ya ndimu,
machungwa, nyanya. Vitamin C itasaidia uterus kuwa na nguvu ya kutosha ili
kufanya kazi vizuri wakati wa labor, pia itasaidia kulinda mwili na infection na
kusaidia kuabsorb iron kwenye mwili.
Siagi na
mafuta: Serving tatu za maparachichi, siagi, olive oil au flax seed oil.
Matunda
yenye rangi ya njano au orange: Huupa mwili vitamin A hii husaidia kulinda
kibofu na figo kupata infections.
Maini kama unaypenda ni mazuri kwa protein pia.
Kunywa maji mengi ya kutosha. Maji huchangia kwa asilimia 75 ya
uzito wa mtoto wako atakapozaliwa. Usipopata maji ya kutosha utaishiwa na nguvu
kwa asilimia 20 na kupata matatizo ya dehydration na kichwa kuuma.
`
Chumvi ya kutosha kusaidia kuzunguka kwa damu kutoka
mwilini kwenda kwenye placenta. Kutopata chumvi ya kutosha kunaweza kusababisha
miguu kuuma na uchovu.
Kwenye sehemu ya pili tutaongelea virutubisho kadhaa na umuhimu wake kwa mama mjamzito na mtoto.
Na vipi kuhusu maini ya nguruwe kwa mama mjamzito?
ReplyDelete