Wanawake
wengi huwa wanaogopa kuongezeka uzito sana wakati wa ujauzito kwa sababu ya
kupoteza mvuto wao baada ya kuzaa. Kitu ambacho unabidi ukumbuke ni kwamba
ukila chakula chenye afya kwa mama mjamzito basi uzito wote utakaoupata kwa
wakati huu ni ule ambao mwili wako unauhitaji.
Katika
kipindi hichi mwili hufanya kazi kubwa sana katika kutengeneza viungo vya mtoto
na pia katika kuujenga mwili wa mama ili uweze kusupport na kumtunza mtoto kwa
kipindi kizima cha ujauzito.
Wamama
wengi husikia njaa sana wanapokuwa wajawazito na huwa na hamu kubwa ya kula hii
ni njia ya mwili kumkumbusha mama kutosheleza mwili kwa ajili ya kipindi hiki
maalum. Pamoja na hayo usichukulie hii kama sababu ya kula chakula chochote
kile. Mama anabidi apate virutubisho vizuri vinavyotakiwa kwa afya yake na
mtoto.
Kula chakula ambacho kina diet na balanced especially kwamama mjamzito ambacho kina protein ya hali ya juu. Usile vyakula vyenye mafuta
mengi, sukari au vyakula vya junk food.
Kitu muhimu kwa mama mjamzito ni kuhakikisha hali vyakula
vilivyotengenezwa viwandani yaani processed food na junk food, pia vyakula
ambavyo haviko natural kwani hivi vinasababisha unene bila kuupa mwili au mtoto
virutubisho vya kutosha.
Hivyo mama anahitaji ahakikishe kuwa anakula vyakula natural
vilivopikwa nyumbani vyenye protein ya kutosha. Kumbuka ubongo wa mtoto na wa
mama umetengenezwa na 75% ya mafuta ya cholesterol. Na ni muhimu sana mama
kutosheleza mahitaji yake ya cholesterol kutoka kwenye vyakula vyenye protein
ya juu kama vile maziwa. Ndio maana maziwa ni muhimu sana kwa mtoto anayekua
ili kuutengeneza ubongo wake.
Je, unapopima uzito huo uzito unaongezeka mwilini huenda
wapi? Kumbuka sio uzito wote unaoongezeka wakati wa ujauzito ni uzito wa
kunenepa bali:
- 7.5 – 8 pound ni uzito wa mtoto
- 2 pound ni za amniotic fluid( yale maji ambayo yanamlinda mtoto ndani ya uzazi)
- 1.5 – 2pound ni placenta( mfuko wa uzazi)
- 1.5 -2pound zitaenda kwenda kwenye maziwa kutayarisha utengenezaji wa chakula cha mtoto atakapozaliwa
- 3lb ni damu ambayo itaongezeka mwilini kuhakikisha unadamu ya kutosha
- 2 – 2lb misuli ya uzazi
- 4 pound maji
- 8 pound ni mafuta ya akiba kutosheleza mwili na kukupa nguvu ya kila siku.
Kwa mara
nyingi mama mjauzito anashauriwa aongeze uzito kati ya 25 pound mpaka 35 pounds
lakini usifuatishe sana hizi namba kwani kila mtu ni tofauti. Ili mradi unakula
chakula bora kwa mama mjamzito basi usiwe na wasiwasi wa kuongezeka kwani mwili
wako unajua ni kiasi gani unahitaji kwa ajili yako na mtoto.
Pia
ukumbuke kuwa kutokuwa na uzito wa kutosha utasababisha mtoto kuzaliwa na uzito
mdogo ambayo ni chini ya 5 pounds hii inaweza kusabibisha mtoto kuzaliwa na
magonjwa au kushindwa kukua vizuri au kuzaliwa njiti.
Pia
ukiongezeka uzito kupita kiasi kutafanya mtoto awe na uzito mkubwa kupita kiasi
kitu ambacho kitasababisha kuongezeka muda wa labour, matatizo ya kuzaa, kuzaa
kwa operesheni au c-section.
Hivyo ni muhimu sana mama kubalance na kuongezeka kwa uzito unaotakiwa kwa afya yake na mtoto.
Pamoja na
kula chakula bora kwa mama kumbuka kupata mazoezi maalum ya mama mjamzito ya
kutosha kila siku. Hii itasaidia mwili wako kutumia virutubisho vya chakula
vizuri na itasaidia pia pale utakapozaa mwili kurudi kiurahisi zaidi.
Kuhusiana
na upunguaji wa uzito wa uzazi, ni kweli kila kukicha tunasikia story za watu
maarufu au macelebrity ambao wamepungua sana pale wanapotoka kuzaa na hivyo wanawake
wengi huwa na dhamira ya kupungua tu pale watakapozaa. Ila ni vizuri kukumbuka
kuwa ulitumia miezi tisa kuongezeka mwili wako ili kujitosheleza wewe na mtoto
hivyo vile vile jipe japo miezi tisa ili upungue.
Sasa
nitashare personal story yangu, naweza kusema baada ya kuzaa mtoto wangu uzito ule wa placenta, maji, mtoto ulisababisha uzito wangu upungue kwa
kiasi kikubwa na mazoezi niliyokuwa nikiyafanya wakati wa ujauzito na vile vile
kunyonyesha kulinisaidia sana.
Nilirudi
katika uzito wa zamani hadi nikapatiliza, mwenyewe nilifurahi sana. Lakini
nilikuwa naambiwa labda sili vya kutosha. Lakini hiyo haikuwa sababu kwasababu
nilikuwa nakula sana na appetite yangu ilikuwa kubwa mno, ni mwili tu ulikuwa
unajaribu kujirekebisha baada ya kumaliza kazi moja na kujitayarisha kwenda
katika kazi ya pili ya kumnyonyesha mtoto aliyezaliwa.
Pia kumbuka katika muda
huu mama anakuwa hapati usingizi wa kutosha kwasababu ya kuamka kumhudumia
mtoto na wengine huwa hawana wasaidizi nyumbani hivyo wanabidi pia waendelee
kufanya kazi muhimu za ndani. Hivyo mwili pia bado unajaribu kujijenga kwa
sababu ya uchovu na kazi ya kuzaa.
Ni katika
kipindi hiki mama anaweza kudhani kuwa ameweza kumaintain kurudi katika uzito
wake wa zamani.
Lakini kitu
kilichotokea baada ya hapo ni kuwa kwa vile nilikuwa nanyonyesha appetite yangu
iliongezeka kwa kiasi kikubwa ili kutosheleza kutengeneza chakula cha mtoto na
pia kuuguza mwili kutokana na kazi iliyoifanya ya kuzaa.
Basi mtoto
alipoacha kunyonya baada ya kama mwaka mmoja na nusu hivi mimi nilikuwa
nishazoea kula kiasi kikubwa kupita zamani. Sasa mtoto kaacha kunyonya
na mimi nakula kama vile bado natengeneza chakula cha mtoto. Basi hapo katika
hicho kipindi ndio nikaanza kunenepa, hadi mwili ulipobaini kuwa hauhitaji tena
kutengeneza chakula cha mtoto na matumizi kupungua ndio appetite kupungua na ndio
mwili ukaanza kurudia tena hali ya awali.
Katika muda huu mama anakuwa tayari anaweza kurudi katika
diet yake ya kawaida na kufanya mazoezi ili kufikia lengo lake la kupungua kwa
usalama zaidi.
Je wewe kama umeshazaa unaexpereince gani katika uongezekaji wa uzito? unaweza kutuma comment yako hapo chini au kutuma email kama unataka kuuliza swali mwanamkeuzazi@gmail.com
No comments:
Post a Comment