Monday, May 14, 2012

Maumivu mbali mbali ya tumbo kwa mama mjamzito : Swali Kutoka Kwa msomaji

Ok wapenzi leo nimepata swali kutoka kwa msomaji mwenzenu. Yeye Anauliza...

Hello, Pole na shughuli,

Mwanamke anapokuwa na tatizo la kuumwa tumbo sometimes (linakuwa linanyonga) hasa hasa usiku ikiwa ana pregnancy ya miezi miwili...tatizo nini?

Ahsante.
Kuna sababu kadhaa ambazo zinaweza kusababisha maumivu ya tumbo kwa mama mjamzito, kabla ya kuelezea kwa undani zaidi sababu mbali mbali za maumivu haya ningependa tu kusema kwa ushauri wangu, mama asikiapo maumivu yoyote ambayo si ya kawaida ni vizuri kukutana na daktari maalum wa ujauzito OBGYN kwa ushauri zaidi kama hamjafanya hivyo tayari ili tatizo liangaliwe na daktari kwa umakini na undani zaidi. 

Ni vigumu sana kutoa ushauri maalum bila kufahamu data nzima na historia ya afya ya mwanamke huyo, kwa ajili ya hilo hapa nitatoa tu sababu kadhaa kijuu juu. 


Mara nyingi kuna tofauti kubwa katika maumivu ya tumbo katika miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito(first trimester) na miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito(third trimester). 

Kwanza kabisa siku kadhaa baada ya utungaji wa mimba mama anaweza kupata maumivu ya tumbo(implantation cramping) pale yai linapojishikisha kwenye ukuta wa uterus. Hii inatokea siku saba baada ya ovulation. Wakati mwingine damu kidogo itaonekana katika kipindi hiki. Sio wanawake wote wanapata maumivu haya. Maumivu haya yanaweza kuendelea kwa kipindi kizima cha ujauzito katika kutayarisha uterus kuhifadhi mtoto. 

Pia kabla ya wiki kumi na mbili 12 au miezi mitatu ya ujauzito mama anaweza akasikia maumivu kutokana na kutanuka kwa misuli iliyo chini ya uterus inayoongezeka na kujivuta na kuongeza nafasi ili mtoto apate nafasi ya kutosha kadri anavyoongezeka uzito na anavyokua. Maumivu haya yanaitwa Round Ligament Pain. Mara nyingi wamama ambao ni mama kwa mara ya kwanza au hawajazaa kwa kipindi kirefu watayasikia maumivu haya. Maumivu haya mara nyingi huisha baada ya miezi mitatu lakini yanaweza kuendelea mpaka mwisho wa ujauztio kutokana na maumbile ya mwanamke. 

Jinsi ya kupunguza maumivu ya Round Ligament au kutanuka kwa misuli. 

 1) Fanya Zoezi la Pelvic Rocking kama tulivyoongelea katika maada zilizopita 

 2)Kama ulikuwa unafanya shughuli: simamisha shughuli ulizokuwa ukifanya na egemea kuelekea upande wa maumivu kwa muda mpaka maumivu yatulie. Kama ulikuwa umelala amka halafu egemea upande wa maumivu vile vile mpaka maumvu yatakapo isha au kupungua kwa kasi. 

3) Wakati unaendelea na shughuli zako za kila siku au wakati wa kulala punguza kugeuka kwa nyendo kali (sharp movements).

4) Jaribu kupata kitafunio chenye afya kwenye kundi la vyakula bora au kunywa maji. 

5)Kuoga maji ya moto au uvuguvugu yanaweza kupunguza maumivu.

6)kufanya zoezi la kuvuta pumzi (abominal breathing) 

Maumivu mengine ambayo huwa ya kawaida yanayoweza kutokea kwa mama mjamzito ni maumivu feki ya labor yaani Braxton Hicks Contraction. Haya maumivu huwa yanatokea kuanzia miezi minne ya ujauzito.

Maumivu haya yanakuwa kama maumivu ya labor ila yenyewe hayaendelei mpaka labor, yanatokea tu kutayarisha mwili na labor. 

Maumivu mengine ya tumbo ambayo ni ya kawaida wakati wa ujauzito ni pamoja na kukosa choo au kupata choo kigumu(constipation) au kiungulia(heartburn) na tulishaongelea jinsi ya kukabiliana na haya katika maada zilizopita. 

Wakati mwingine kuumwa kwa tumbo kunaweza kutokana na magonjwa au hali mbaya kwa mama ikiwa pamoja na yafuatayo: 

1) Miscarriage(au kupoteza mtoto kabla ya muda)kipindi cha trimester ya kwanza (miezi mitatu ya kwanza). Kama mama anasikia maumivu kama yale ayapatayo wakati wa siku zake za mwezi(menstruation) ikifuatiwa na damu ni vizuri kumuona daktari mara moja. 

2)Urinary Tract Infection: Mama akiwa anasikia maumivu wakati wa haja ndogo, hajisikii vizuri, ana homa, kutojisikia kula ni vizuri kwenda kwa daktari kupima ili kupata matibabu na dawa maalum kuponya ugonjwa huu. 

3)Vidonda vya tumbo husababishwa na acid nyingi kupita kiasi tumboni. Mama ale vyakula visivyo na acid kama maumivu yakizidi akutane na daktari. 

4)Appendix: Mama akutane na daktari kupima na kupata matibabu. 

5)Ectopic Pregnancy: Ujauzito kutunga nje ya mfuko wa uterus. Mama anabidi akutane na daktari mara moja. 

6)Fibroids: kama ulikuwa na fibroids kabla ya ujauzito au una historia ya ugonjwa huu katika familia yako ni vizuri kukutana na daktari na kupata ushauri zaidi.

Magonjwa yaliyotajwa hapo juu ni baadhi tu ya magonjwa yanayoweza kusababisha kuumwa kwa tumbo kwa mama mjamzito.

Cha muhimu kama mama anamaumivu makali tumboni ni vizuri tu kufanyiwa check up na daktari hasa hasa mtaalamu wa wamama wajawazito(OBGYN) kuhakikisha kila kitu kiko sawa.

Asante sana kwa swali lako.

Kwa wasomaji wengine kama mna maswali mnakaribishwa kuyatuma mwanamkeuzazi@gmail.com


6 comments:

 1. NAITWA NAKY NINA UMRI MIAKA 26 NINASUMBULIWA NA TUMBO SANA MAENEO YA CHINI YA KITOVU LINAUMA KAMA NINA BLEED NA NIKIPIMA NAONEKANA NINA U T I KIDOGO SANA NA UKIANGALIA MIMBA HAIONEKANI SS NIFANYE NINI ILA BADO SIJAPITISHA SIKU ZANGU NISAIDIENI MADOKTA NATESEKA.

  ReplyDelete
 2. Maumivu upande kushoto kwako chinos tumbo

  ReplyDelete
 3. Ahsante Sana doctor na mm ni mojawapo Wa hayo matatizo... Nanilienda kupima nikaambiwa na uvimbe kwenye mayai Nasasahv nipo kwenye dozi ya sindano guys naomba mnisaidie kwa Yoyote anaejua dawa ya kienyeji ya ili Tatizo anisaidie... Nina ujauzito Wa wiki Saba sasa

  ReplyDelete
 4. Nina mimba ya week lkn tumbo linauma na mwili kuisha nguvu

  ReplyDelete