Kwa kawaida mwanamke
anaweza kusikia uchovu sana hasa hasa katika trimester ya kwanza ya
ujauzito (miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito) hii ni sababu mwili unafanya kazi
nyingi mojawapo ikiwa kutengeneza placenta (nyumba ya mtoto) mwili pia
unatengeneza damu nyingi kuwatosha mama na mtoto na moyo wa mama unafanya kazi
ya ziada kuhakikisha damu inazunguka sawa sawa kwa mama pamoja na mtoto. Tulishaongelea jinsi mama anaweza kukabiliana na uchovu kwa kipindi hiki kwenye maada zilizopita.
Baada ya miezi hii ni
kawaida kwa mama kuanza kupata matatizo ya kushindwa kulala vizuri au kupata
usingizi usiku.
Sababu mojawapo ni
pamoja na uongezekaji wa uzito wa mtoto ambao unaweza kusabiabisha mama kukosa
position nzuri ya kulala hasa hasa kwa wale ambao wamezoea kulalia mgongo au
tumbo. Pia kugeuka wakati wa kulala kunawia vigumu zaidi.
Sababu nyingine ni
kuongezeka kwa safari za kwenda haja ndogo. Hii inasababishwa na figo kuongeza
kazi yake ya kuchuja damu kwa sababu damu imeongezeka mwilini mpaka asilimia
30 hadi 50 kuliko kabla ya ujauzito hii inamaanisha kazi hii huongeza kiasi cha
mkojo unaotengenezwa.
Pia kadri mtoto anavyokua anaweka uzito kwenye kibofu cha
mama kitu kinachosababisha kusikia kwenda haja ndogo mara kwa mara. Na kama
mtoto anakuwa amechangamka zaidi kipindi cha usiku basi utajisikia kwenda
chooni zaidi katika kipindi hiki.
Kuongezeka kwa mapigo
ya moyo kunaweza kukosesha usingizi. Mapigo yataongezeka kwasababu moyo
unafanya kazi ya ziada kusukuma damu iliyoongezeka mwilini mwa mama.
Kutoweza kupumua
vizuri pia kunaweza kusababisha kutopata usingizi. Mama atashindwa kupumua kwa
sababu ya kubadilika kwa hormone mbali mbali mwilini ambazo zitamfanya aheme
kwa nguvu zaidi. Hii itamfanya mama ajisikie kama anashindwa kupumua vizuri.
Kadri mtoto anvayokua na kuongezeka pia anachukua nafasi ya ziada kwenye uterus
na uterus inaongezeka mpaka kufikia kuweka pressure kwenye eneo la mapafu kitu
ambacho kinaweza kumkosesha mama kupumua vizuri.
Miguu na mgongo kuuma
pia kunaweza kumkosesha mama usingizi. Maumivu haya yanasababishwa na uzito
unaongezeka wa mtoto pamoja na hormone maalum ya relaxin. Hormone ya relaxin
inalegeza misuli mbali mbali ya mama kwenye sehemu ya mgongo ili kumtayarisha na
kazi ya kujifungua kulegea kwa hii misuli kutasababisha mama kuumia na kusikia
maumivu kiurahisi zaidi katika maeneo haya hasa hasa mgongoni. Tulishaongelea jinsi ya kukabiliana na maumivu ya mgongo hapo nyuma.
Kiungulia na constipation (kukosa choo au kushindwa kwenda chooni) kama tulivyoongelea kitambo kunaweza kumkosesha usingizi
mama. Mara nyingi wakati wa ujauzito zoezi zima la kusaga chakula linachukua
muda zaidi ili kuhakikisha chakula kinakaa tumbo kwa muda mrefu zaidi hii
inaweza kusababisha kiungilia na constipation. Pia uongezekaji wa mtoto
kunaweka pressure au uzito kwenye tumbo au utumbo mkubwa ambao utasababisha
matatizo haya pia.
Wakati wa ujauzito
wanawake wengine wanakuwa na ndoto mbaya au ndoto ambazo zinafanana na ukweli
ambazo zinaweza kumsababisha mama kushindwa kulala vizuri. Wanawake pia kuwa na
stress za aina yoyote labda kwa ajili ya kuwa na mawazo ya hali ya mtoto au
uoga wa kuzaa au hata matatizo yoyote maishani mwake kunaweza kumkosesha mama usingizi.
Jinsi ya kulala wakati wa ujauzito.
Ni vizuri mwanzoni wa
ujauzito kujizoesha kulala positon ya upande wakati miguu imekunjwa. Kulala
namna kutamsaidia sana mama hasa pale ujauzito utakapoongezeka. Kulala kwa upande kutasaidia uzito wa mtoto kutoegemea kwenye mshipa au ateri kubwa wa
moyo, hivyo moyo utaweza kufanya kazi yake ya kusafirisha damu kwa urahisi
zaidi.
Madaktari wengine
hushauri mama kulalia upande wa kushoto kwa sababu ini liko upande wa kulia
kulala upande wa kushoto kutasaidia uterus kutoegemea upande huo. Pia damu
itaweza kusafirishwa kwa ufanisi zaidi kwenda kwa mtoto katika upande huu.
Ukilala tumia mito kusupport mgongo na magoti Kuweka mto mkubwa chini ya tumbo na
katikati ya miguu unaweza kusaidia na kuweka mto mdogo chini ya mgongo.
Kumbuka hata kama
unapata shida kulala mama mjamzito hashauriwi kunywa dawa yoyote ya kusaidia
kuongeza usingizi.
Ili kupata usingizi mzuri.
Usinywe kahawa, na soda au vitu vyenye sukari kama chocolate
au vitafunio vyovyote vyenye sukari. Viondoe kabisa kwenye
diet yako hasa hasa wakati wa asubuhi au mida ya karibia na mchana.
Hakikisha unapata
glass 8 za maji kwa siku lakini usile vyakula vizito wakati wa usiku kabla ya
kulala au kunywa vinywaji vingi. '
Jaribu
kula breakfast nzito na lunch nzito
halafu kula chakula kidogo zaidi wakati wa dinner. Kama unasikia kichefu chefu
usiku kula mikatie mikavu( crackers ) kabla ya kwenda kulala.
Jaribu kuwa na ratiba
rasmi ya kuamka na kwenda kulala ili mwli uzoee.
Hakikasha unapata mazoezi ya
kutosha kwenye siku yako hii itafanya mwili uchoke na kupata usingizi mzuri usiku.
Lakini usifanye maoezi makali kabla ya
kwenda kulala. Badala yake jaribu kufanya zoezi la relaxation au yoga.
Pia kuoga maji ya moto dakika 15 kabla ya
kulala kutasaidia kupata usingizi murua.
Kabla ya kulala unaweza
kunywa vinywaji vya moto kama maziwa
ya moto na asali au chai aina ya chamomile kusaidia kurelax.
Jaribu kupata usingizi wa mchana kupunguza uchovu
Muombe mumeo au mtu wa karibu kwako kifamilia kukusaidia
kurelax na kuweka mood sawa wakati wa kulala. Hii ni pamoja na kupata massage ya miguu mgongo ili kusaidia
kurelax na kupata usingizi.
Kama unaumwa na miguu
simamia miguu ili kupungza maumivu halafu hakikisha unapata calcium ya
kutosha kwenye diet yako. Angalia mada zilizopita kwa maelezo zaidi.
Kama unashindwa
kulala unaweza kusoma kitabu, sikiliza mziki taratibu murua, angalia tv au
fanya kitu ambacho kitakufurahisha katika kipindi hiki mpaka upatapo usingizi
tena.
No comments:
Post a Comment