Sunday, April 29, 2012

Birth Affirmations - Maneneo ya kumpa moyo, ujasiri na kumfariji mama mjamzito

Tutakuwa na kipengele kipya cha "Birth Affirmations", haya ni maneno mazuri ya kumpa mama mjamzito faraja na moyo wa kutokuwa na uoga na uzazi bali kufurahia wakati huu muhimu katika maisha yake na kumpa ujasiri kuwa anaweza kukabiliana na machungu ili kuweza kufikia kilele cha kumleta mtoto aliyebarikiwa naye duniani.

Ni vizuri kila mara au kila siku kuyasoma maneno haya au kuyafikiria kama tulivyoongelea kwenye kipengele cha relaxation. Hii itamsaidia kumpa ujasiri na kutokuwa na uoga bali kuwa na matumaini na furaha.

Hali ya kutokuwa na uoga kutamsaidia mama mjamzito kuweza kulegeza misuli yake na kurelax wakati wa labor hali ambayo itapunguza maumivu kwa kiasi kikubwa na kusaidia zoezi zima la kuzaa kwenda kwa urahisi zaidi.


 

 

No comments:

Post a Comment