Tuesday, May 29, 2012

Kuumwa kwa kichwa wakati wa ujauzito


Wanawake wengi hupata tatizo la kuumwa kwa kichwa wakati wa ujauzito. Hili tatizo huweza kutokea wakati wowote wa ujauzito lakini mara nyingi hutokea wakati wa trimester ya kwanza (miezi mitatu ya kwanza) na trimester ya tatu (miezi mitatu ya mwisho) ya ujauzito.


Katika trimester ya kwanza kuumwa kwa kichwa mara nyingi husabababishwa na kuongezeka kwa hormone na damu inayosukumwa mwilini.

Kuumwa kwa kichwa kunaweza kuongezeka zaidi pale mwanamke mjamzito akiwa na stress, kukosekana kwa usingizi, uchovu, mafua, kuwa na low blood sugar(sukari isiyotosha kwenye damu), ukosekanaji wa maji ya kutosha mwilini(dehydration),  kwa wale waliozoea kunywa kahawa kuacha kunywa kahawa kunaweza kusababisha kuumwa kwa kichwa.

Kuumwa kwa kichwa wakati wa trimester ya mwisho husababishwa na kuongezeka kwa uzito unaoweka stress kwenye mwili, mwili kutokuwa balanced, pamoja na wanawake wengine kuwa na high blood pressure wakati wa ujauzito(preeclampsia).

Mara nyingi mama mjamzito hashauriwi kunywa dawa zozote zile kwa kipindi hiki kwasababu kuna uwezekano wa dawa kupokelewa na mtoto na kumdhuru kwa namna moja au nyingine. Hii ni sababu maalaamu kujaribu kutumia njia natural kupunguza maumivu yoyote yale mama anayopatwa nayo kwa kipindi hiki.

Jinsi ya kupunguza au kuondoa maumivu ya kichwa wakati wa ujauzito.

Jaribu kutuliza misuli ya uso na kupumzika.

Uwe makini na madawa ya aspirin na jamii za dawa hii, kwa vile dawa yoyote uinywao inaweza kumuaffect mtoto.

Ukisikia maumivu jaribu kunywa maji glass 2 - 3, kwasababu wakati mwingine maumivu husababishwa na kukosa maji ya kutosha mwilini.

Fanya zoezi la kutembea halafu kunywa maji mengi ya kutosha.

Chunguza vyakula unavyokula unaweza ukawa unapata reaction.

Pumzika vya kutosha na kupata mazoezi ya relaxation.

Fanya mazoezi mara kwa mara kama unavyotakiwa kwa mama mjamzito.

Kula chakula chenye afya kwa mama mjamzito.

Unaweza kuweka kitambaa cha moto kwenye eneo la macho, pua na kichwa kama kuuma kwa kichwa kunasababishwa na mafua au weka kitambaa cha baridi kwenye sehemu inayouma kama ni maumivu ya kichwa ya kawaida.

Hakikisha unabalance kiasi cha sukari kwenye damu(blood sugar)yako kwa kula kiasi kidogo cha chakula kila baada ya muda mfupi badala ya kusubiri kwa muda mrefu halafu kula mlo mkubwa.

Ukipata massage ya shingo, mabega na uti wa mgongo itapunguza stress na kupunguza maumivu ya kichwa.

Pumzika kwenye chumba chenye giza halafu jaribu kuvuta pumzi na kuachia ili kuondoa stress mwilini.

Oga maji ya moto au baridi.

Baadhi ya vyakula vinaweza kuchangia kuumwa kwa kichwa. Unaweza kujaribu kuvitoa kwenye diet yako kuona kama vitasababisha kupunguza maumivu ya kichwa.

Hivi vyakula ni pamoja na:


Chocolate
Vinywaji vikali
Mtindi, jibini, sour cream
Karanga
Mikate yenye yeast
Nyama zilizowekwa kemikali ili kuzisaidia kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika.(processed milk)

Ongea na daktari kama umejaribu vitu hivi na bado maumivu yapo au yanazidi au kuumwa kwa kichwa kunaambatana na kizungu zungu, kuvimba kwa mwili, maumivu kwenye maeneo ya juu ya tumbo au
kuongezeka kwa uzito ghafla.

No comments:

Post a Comment