Friday, May 25, 2012

Kuwa kwenye mood mbaya kwa mama Mjamzito



Mara nyingi wanawake wakati wa ujauzito wanabadilika sana kihisia. Utakuta kwa muda mfupi kafurahi halafu umefanya kitu kidogo umemkasirisha. Wakati mwingine wanaweza wakawa wanahasira au kuwa kwenye mood mbaya bila sababu. Hiki ni kitu cha kawaida kabisa. Kumbuka mwanamke anakuwa katika kipindi ambacho mwili hukabiliana na mabadiliko mengi ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya kimwili, hormone, uchovu, kubadilika kwa usagaji na utengenezwaji wa chakula mwilini pamoja na stress mbali mbali za maisha. Haya yote kutokea kwa wakati mmoja yanaweza kusababisha kubadilika wa hisia zake na kuchoka pia.

 
Ni vizuri kurelax, kufanya mazoezi na kula chakula chenye afya njema kwa mama mjamzito ili kumpa mwanamke nguvu na kusaidia na hisia. 

Wakati wa ujauzito ni wakati mzuri wa kutafakari maisha kwa ujumla, kusikiliza hisia na kuwa karibu na nafsi yako ikiwa kwa njia ya maombi na meditation. Hii itasaidia roho kuwa nyeupe. Si wakati mzuri wa kuwa na mawazo na wasi wasi kwa mambo mengi yanayoendelea katika maisha ikiwa katika mahusiano, kazi n.k

Kubadilika kwa hormone, kuongezeka kwa damu na maji mwilini na kemikali mbali mbali zinaweza kutuma message kwenye ubongo ambayo inaweza kubadili hisia za mwanamke ghafla. Ni kitu cha kawaida ambacho kitakuwa kinakuja na kuondoka.

Mara nyingi mwanamke hupatwa na haya matatizo kuanzia wiki ya sita ya ujauztio mpaka wiki ya kumi halafu linaweza kurudi tena katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito (third trimester).


Ili kupunguza stress na kusaidia hisia za mwanamke mjamzito ni vizuri:

 

Kupumzika vya kutosha. Jaribu kutenga muda maalum kwenye siku yako ambayo unaweza kurelax na kutokusumbuliwa na kitu au mtu yoyote na kufanya yale upendayo. Inaweza ikiwa pamoja na kusikiliza mziki mzuri wa kurelax hisia,kupata massage, kusoma kitabu, kutafakari, kuangalia tv/movie, kufanya maombi, kuabudu, kufanya mazoezi aina ya yoga, kufanya mazoezi ya relaxation kama tulivyoelezea kwenye maada zilizo pita, meditation, kusoma maneno mazuri ya kukufariji kama yale ya birth affirmations au chochote kile ambacho unakipendelea ambacho huwa kinakufurahisha. Katika kipindi hiki cha siku yako usiwe na wasiwasi kuhusu kumaliza kazi zako mbali mbali ikiwa pamoja na majukumu ya ndani au kazini au chochote kile ambacho kinakutia wasiwasi. Kumbuka mtoto akizaliwa utakuwa una kazi nyingi za ziada za kufanya hivyo jaribu kutunza nguvu zako kwa ajili ya kipindi hiki muhimu kwako, kwa mtoto na familia kwa ujumla.Pale usikiapo hisiakuwa mbaya ni vizuri kubadili kitu ulichokuwa unakifanya na jaribu kufanya kitu kitakacho kuchangamsha.


 
Jaribu kutenga muda wa kuwa na mumeo, mtu wa karibu kwako, ndugu na marafiki. Huu muda uwe tu wa kufurahia maisha au kuongelea mambo mazuri kwenu. Pia kama kuna kitu kinakusumbua ni vizuri kuongea na wale wa karibu kwako na kuongea nao kwa utaratibu ili kupata ufumbuzi au suluhisho. Pia ili watu karibu wako waweze kuelewa jinsi vile unavyojisikia.

Pata muda wa kwenda nje na kutembea kwenye sehemu yenye hewa safi, ikiwa sehemu yenye miti mingi na oxygen au hata sehemu yenye maji kama baharini au ziwa. Hii itasaidia kurekebisha hisia, kubadili mandhari na pia kupata muda wa kutafakari. Kutembea pia ni mazoezi mazuri sana kwa mama mjamzito.

Hakikisha unafanya mazoezi. Dakika 10 mpaka 30 tu za mazoezi kila siku au mara kwa mara zinatosha kukupa nguvu ya kutosha, kuzuia kuchoka na kuwa depressed. 

Hakikisha unakula chakula kizuri chenye afya kwa mamamjamzito. Mwili wako unahitaji protein ya kutosha na viritubisho mbali mbali ili kumtosheleza mtoto na wewe mwenyewe. Ukikosa kiwango cha kutosha basi unaanza kupata vishawishi au kutamani vyakula vyenye sukari. Kula vyakula vyenye sukari nyingi, kahawa, chumvi, junk food (vyakula vyenye kemikali) vinachangia kwa kiasi kikubwa kutoa kemikali mwilini ambazo zinauwezo wa kubadili hisia zetu. Kula vyakula vya aina hii husababisha kupanda na kushuka kwa sukari kwenye damu, kuchoka na wakati mwingine depression. Vyakula hivi mara nyingi vinakufanya ufurahi au ujisikie una nguvu na furaha haraka na kwa mara moja (sugar high) halafu baada ya muda mchache unakuwa depressed au kuchoka pamoja na kuwa na mood mbaya.

Jaribu kutoa kabisa kwenye diet yako sukari nyeupe, vyakula vyenye fructose, maple syrup au  asali. Kula vitafunio vyenye protein ya hali ya juu kama mtindi, karanga, samaki aina ya dagaa/sardines na jibini/cheese.

Vinywaji vizuri amabavyo vinaweza kusaidia kurekebisha hisia na kukuchangamsha:

 

Chai ya Raspberry ikiongezwa na peppermint au spearmint husaidia kurekebisha hisia, kuchangamsha na kukupa nguvu.

Chai ya Raspberry
Chupa ya Peppermint
Chupa ya Spearmint






vinywaji vya mimea ya burdock, blessed thistle na sarsaparilla ni michungu ila kunywa hii mara moja moja husaidia pia kurekebisha hisia.

Chai ya mmea wa Burdock
Maji ya mmea wa Blessed thistle
Kinywaji cha sarsaparilla
 
Maji ya motherwort inasaidia kurelax bila kukufanya uwe na usingizi ni nzuri ukiwa kazini au hata nyumbani ukisikia kama stress zimekuzidia. Weka vitone vitano kwenye glass ya maji. Baada ya dakika 15 utasikia nafuu. Unaweza kunywa kila baada ya masaa mawili. Hii itafanya vizuri zaidi ukiinywa wakati wako uliotenga kurelax. Hii haitakiwi kuinywa kila wakati kwa sababu kunauwezekano wa kuizoea na kutoweza kurelax bila kuinywa.  Inafaa tu kunywewa mara moja moja pale unaposikia kuzidiwa na stress.

maji ya motherwort
 
Maji ya mmea wa skullcap yanasaidia usingizi mzuri unaweza kutumia vitone 30 kama umeinunuwa dukani au vitone 5 hadi 15 kwa mmea fresh nusu saa kabla ya kulala. Unaweza kunywa vikombe viwili kwa siku. Kama hisia zako ni mbaya sana.

maji ya mmea wa skullcap
 
Kama hizia zako zimezidi kuwa mbaya kiasi cha kupata depression ni vizuri kuonana na mtaalamu.

Dalili za Depression hutambulika pale:

  • Hisia mbaya zinaendelea kwa zaidi ya wiki mbili mfululizo.
  • Hupati usingizi usiku kwa ajili hii.
  • Huwezi kula vizuri.
  • Mawazo yamekuelemea mpaka huwezi kuconcentrate kwa muda.
  • Uwezo wako wa kukumbuka umepungua

No comments:

Post a Comment