Tatizo la kuvimba kwa
maziwa na kuuma wakati wa ujauzito linatokana na kuongezeka kwa hormone za progesterone
na estrogen mwilini.
Kitu cha kwanza kabisa ni kuzingatia kuvaa bra
inayokutosha. Mara nyingi wanawake wanaendelea kuvaa bra za zamani wakati
maziwa yameongezeka. Hivyo wanakosa support ya kutosha. Uvaaji wa bra yenye
support ya kutosha wakati wa mchana hata usiku utasaidia kupunguza maumivu na
kukufanya uwe comfortable zaidi.
Pia usivae bra zenye chuma ndani(underwire, ukilala hakiksha unayapa support ya kutosha kwa kulala
vizuri.
Unaweza kupaka mafuta ya lanolin kwenye ngozi ya maziwa
yaliyovimba.Hasa hasa kwenye sehemu zinazowasha au zilizokauka na kuanza
kuchubuka.
Mafuta ya Lansinoh |
Kupunguza maumivu jikande na maji ya moto au oga maji ya moto hakikisha maji
yako ni chini ya 100 degree Fahreinheit kwani maji yaliyozidi degree 100 Fahreinheit si mazuri kwa mama
mjamzito.
Pia unaweza kuweka maji ya baridi ya au weka barafu kwenye
kitambaa halafu weka kwenye maziwa yaliyovimba ili kupunguza maumivu na uvimbe.
Usinywe kahawa au vinywaji vyenye cola maana hizi
zinazidisha uvimbe na kuuma. Jaribu kunywa chai maana majani mengi ya chai yana
virutubisho vya potassium hii husaidia kupungza uvimbe. Pia punguza
chumvi kwenye vyakula.
No comments:
Post a Comment