Wakati wa ujauzito mwili hutengeneza asilimia
50 zaidi ya damu na maji maji ili kumtosheleza mama na mtoto. Kuvimba kwa mwili
wa mama ni kitu cha kawaida kwa ajili ya kuongezeka kwa damu mwilini. Na kuongezeka
kwa pressure kwenye mishipa ya miguu na mikono kwa ajili ya ukuaji wa mtoto. Mama
huweza kuvimba usoni, mikono, miguu.
Kuongezeka kwa maji mwili pia husaidia
kulainisha mwili ili kusaidia kuongezeka kwa mwili mtoto anavyozidi kukua, pia
husaidia kufungua misuli ya hips na chini ya tumbo ili kutayarisha njia ili
mtoto aweze kupita.
Kuvimba kunaweza kutokea wakati wowote wa
ujauzito lakini mara nyingi hutokea kuanzia mwezi wa tano
Kuvimba pia kunaweza kusababishwa na:
Joto.
Kusimama kwa kipindi
kirefu.
Kazi nyingi katika
siku yako.
Diet yako ikiwa haina
potassium ya kutosha.
Kunywa kahawa au
vyakula na vinywaji vyenye kahawa kwa wingi.
Diet yako ikiwa na
sodium au chumvi nyingi.
Kuvimba kunaweza kupunguzwa kwa
Kula vyukula vyenye potassium kwa wingi kama ndizi na hasa hasa tunda la
cantaloupe.
tunda aina ya cantaloupe |
Usisimame kwa kipindi
kirefu.
Usikae nje kwa muda
mrefu hasa wakati wa joto.
Ukipumzika elekeza au
egemeza miguu juu.
Vaa viatu ambavyo
viko comfortable na usivae viatu virefu.
Usivae nguo za kubana
hasa hasa kwenye maeneo ya mikono na miguu.
Pumzika vya kutosha.
Pata zoezi la
kuogelea.
Pata mazoezi kila siku lakini usipitilize
Unaweza kujikanda
kwenye sehemu zilizovimba.
Kunywa maji kwa wingi
hii itasaidia kutoa maji mwilini na kupunguza uvimbe. Na jaribu juice natural organic za cranberry na
dhabibu. Nikisema natural au organiz na maanisha zile zilizotengenezwa na matunda asilia na hazijawekwa sukari ya kuongezwa au makemikali.
juice ya dhabibu |
juice ya cranberry |
juice na matunda ya cranberry |
Punguza chumvi kwenye
vyakula na diet yako kwa ujumla.
Ongeza Protein katika diet yako.
Kumbuka wakati mwingine kuvimba ni tatizo la kawaida na
huashiria kuwa ujauzito unaendelea vizuri.
Mwombe mpenzi mumeo au mtu wa karibu nyumbani akupe massage
ya maeneo yaliyovimba na mafuta. Hasa hasa mafuta ya grapeseed(mafuta ya dhabibu) yanaweza kusaidia.
mafuta ya dhabibu |
Zamisha miguu kwenye maji yenye mafuta ya cypress hii husaidia mzunguko wa damu au mafuta ya
lavender na chamomile hizi husaidia kurelax.
mafuta ya cypress |
mafuta ya chamomile |
mafuta ya lavender |
Kuweka majani cabbage kwenye sehemu iliyovimba itasaidia
kutoa maji na kupunguza maumivu.
- Weka cabbage kwenye fridge sio freezer halafu yafute na kitambaa lakini usiyasafishe .
- Weka vipande hivyo kwenye sehemu zilizovimba halafu ziache hapo mpaka zilowe halafu rudia na majani mengine fresh mpaka maumivu yapungue.Unaweza kufanya hivi mara nyingi mpaka pale unapopata nafuu.
No comments:
Post a Comment