Hii topic nilikuwa na dhamira ya kuliongelea hapo mbele na ni mojawapo ya dhumuni la kuanzishwa kwa blog hii, kujadili topic kama hizi.
Jibu ni refu kidogo kwa hivyo naomba muwe na subira katika kusoma jibu kwa vile ni muhimu sana tuelewe mambo haya muhimu. Pia majibu mbali mbali niliyoelezea kwenye topic hii nitaendelea kuyachambua na kuyaongelea kwa kirefu zaidi katika maada nilizoziandaa hapo wiki zijazo.
Kwa hiyo endeleeni kutembelea blogu ili kupata ufahamu zaidi. Na kama mna maswali mnakaribishwa kuyatuma mwanamkeuzazi@gmail.com
Mimi nilikuwa nataka nijue tatizo lililopo kwasasa kwa wanawake wanapoenda kujifungua, njia za uzazi hazifunguki mpaka inafikia hatua mama anaongezewa uchungu ili njia iweze kuongezeka lakini haisadii hili tatizo linakuwa la nini hasa? kwasababu wazazi wetu hawakuwa na matatizo ya kufunguka njia mama akishapata uchungu tu njia inafunga bila shida lakini kwasasa hivi hili ni tatizo kubwa sana kwa wa mama mpaka inafikia hatua mabinti wanaogopa kujifungua kwa kawaida wakiogopa kupata maumivu yake badala yake wanapendelea visu kwa sana.
Kuna sababu mbali mbali zinazosababisha wanawake wa siku hizi kushindwa kufunguka kwa njia ya uzazi na kuwalazimu kupewa madawa kuongeza uchungu au hata kutakiwa kuzaa kwa operesheni/visu/ c-section. Hapa nitajaribu kuchambua kila sababu na ni kwa kivipi hili linachangia.
1. Mazoezi
Wanawake wa zamani walikuwa wakifanya shughuli nyingi sana
kama kutembea kwa muda mrefu ili kufika sehemu wanazotaka. Walikuwa wanafanya
shughuli nyingi za ndani na nje ambazo wanawake wengi wa siku hizi hawafanyi. Shughuli hizi zilikuwa ni mazoezi tosha, zilizokuwa zikisaidia mwili wa
mwanamke kufunguka na kulegea katika kipindi hiki.
Ila wanawake wa siku hizi mara nyingi tunafanya kazi
ofisini, tunaenda kwa magari, unafika ofisini umekaa kwenye kiti, umerudi
nyumbani unakaa tena kwenye kochi ukila chakula umekaa kwenye meza ya chakula
kwenye kiti, kazi nyingi zimerahisishwa na mashine na hata wasaidizi wa nyumba
unaishia kulala tu au kukaa tena kwenye kochi mbele ya tv, computer au simu.
Siku hizi shughuli nyingi za binadamu zinatumia akili na
ubongo zaidi ya mwili. Ndio imerahisisha maisha yetu ya kila siku ila sasa mwili
wetu unashindwa kufanya kazi yake vizuri na unakuwa mzembe.
Ndio maana siku hizi tunashauriwa kutenga muda maalum
kufanya mazoezi ili kufidia kuupa mwili mazoezi ya kutosha. Na ni muhimu sana
kwa mwanamke mjamzito kufanya mazoezi maalum ili kusaidia kupanua na kuongeza
njia ya uzazi. Na sio kufanya mazoezi yoyote yale bali yale muhimu ambayo yatasaidia kuongeza na kupanua njia na misuli maalumu ya uzazi. Katika hili rudini katika maada za nyuma za mazoezi na ratiba za mazoezi zinazotelewa kila wiki kwenye blog hii.
2. Lishe na diet
Siku hizi lisha bora haizingatiwi na watu wengi kama zamani.
Kutokana na kubadilika kwa maisha ya kila siku na kurahisishwa kwa upikaji na
utengenezaji wa chakula mara nyingi hatupati lishe bora.
Watu wengi utakuta wanaenda kazini wanashindwa kuchagua
chakula bora wanakula tu chakula kile ambacho kipo mitaani kwa haraka warudi
ofisini. Uongo mbaya vyakula ni vitamu lakini si vizuri kwa afya zetu.
Mara nyingi vyakula hivi sio vizuri kwa vile wauzaji wa chakula wanafanya biashara utakuta vyakula hivi vina mafuta mengi na fructose ili waweze kuvitengeneza kwa muda mfupi na kuvifanya viwe na ladha tamu. Vyakula hivi haviko balanced yaani havitoshelezi mlo kamili wenye virutubisho vyote muhimu kwa binadamu hasa hasa kwa mama mjamzito.
Mara nyingi vyakula hivi sio vizuri kwa vile wauzaji wa chakula wanafanya biashara utakuta vyakula hivi vina mafuta mengi na fructose ili waweze kuvitengeneza kwa muda mfupi na kuvifanya viwe na ladha tamu. Vyakula hivi haviko balanced yaani havitoshelezi mlo kamili wenye virutubisho vyote muhimu kwa binadamu hasa hasa kwa mama mjamzito.
*(fructose mbaya ni ile ambayo inatumiwa kama sukari na kuongezwa kwenye
vyakula viwandani. Fructose ya aina hii sio ya asilia inakuwa imekuwa
processed. Siongelei ile ambayo iko naturally kwenye matunda)
Kama mama mjamzito anashindwa kupata lishe bora basi mwili
utashindwa kufanya kazi yake vizuri kumtosheleza mama na mtoto.
Mara nyingi
kinachotokea utakuta mama na mtoto wanaongezeka uzito lakini huu sio uzito
mzuri unaowafaa. Hivyo mtoto anaweza akawa mkubwa sana na inawia vigumu kwa
njia ya uzazi kutosha.
Mara nyingine mwili wa mama pia unashindwa kufanya kazi
ipasavyo kwa vile vyakula vingi vya siku hizi vina kemikali na hormone mbali
mbali ambazo si nzuri kwa binadamu na zinauwezo wa kuaffect zoezi zima la kuzaa
ikiwa ni pamoja na ufungukaji wa njia ya uzazi.
Mama mjamzito anatakiwa achukue hatua maalum kupangilia
chakula ikiwezekana aandike kama ratiba na ajaribu kufuatilia chakula gani
anakula kuona kama anapata mlo kamili. Pia ajaribu kuandaa vyakula vyote
mwenyewe na kununua vyakula amabyo ni organic na natural ambavyo havijaongezwa
madawa na kemikali viwandani.
Pia katika hili nilishaongelea virutubisho vinavyotakiwa kwa mama mzjamzito na mlo kamili uweje, kwa maelezo zaidi kwa hili rudini katika maada za nyuma kuhusiana na hili.
3.Jamii kutokuwa na subira na wamama wajawazito pamoja na uingiliaji wa wauguzi katika shughuli nzima ya kujifungua.
Kuna mara kadhaa ambapo hospitali inaweza kutokadiria vizuri
tarehe za kuzaliwa mtoto. Mama, familia, marafiki na hata madaktari
wakifuatilia hizi tarehe kama maandiko kutoka kwa Mungu inaweza ikawa ni tatizo
kwa mama mjamzito pale tarehe au wiki ya kuzaliwa mtoto itakapofika halafu mama
bado hajaingia labor au kuanza kusikia uchungu wa kuzaa . Utakuta familia na marafiki wanaanza kumuuliza mama mbona mtoto bado hajaja hii haimsaidii mama bali humtia woga na wasiwasi kuwa labda kuna tatizo.
Tunabidi tufikirie kama vile ni tunda, hivi sisi tunafahamu
ya kuwa lini tunda ambalo liko kwenye mti litakuwa tayari na kuiva? Ni Mungu pekee ndio
anafahamu. Mara nyingi tunasubiri mpaka pale limeiva halafu linadondoka
lenyewe. Ukijaribu kulitungua kabla halijaiva unakuta chungu na si tamu tena.
Ukiangalia hiyo graph hapo juu inaonyesha miezi ambayo watoto huweza kuzaliwa. Kuna watoto wachache wanaweza kuzaliwa kabla ya miezi tisa kuanzia miezi sita hadi wa tisa. Ila wengi wao kwa kawaida huzaliwa katika miezi minane hadi tisa ya uzazi baada ya hapo unaona kuna uwezekano kabisa watoto wengi kuzaliwa kuanzia mwezi wa tisa hadi wa kumi wa uzazi. Na wengine wachache kwenye mwezi wa kumi hadi wa kumi na moja.
Kwanini makadirio ya siku ya kuzaliwa mtoto huwa mara nyingi si sahihi?
- Kutofautiana kwa mzunguko wa menstruation cycle au mzunguko wa siku za mwanamke. Wanawake wengine wana mizunguko mrefu na wengine wana mizunguko mifupi.
- Ukuaji wa kila mtoto ni tofauti, watoto wengine wanahitaji siku zaidi kuendelea kuwa ndani ya tumbo la mama.
- Wamama wengine wanapoulizwa lini ilikuwa siku ya mwisho wa hedhi ili kukadiriwa huwa hawana kumbukumbu sahihi.
- Ndiyo maana tunabidi tuchukulie haya kama makadirio na siyo siku maalumu ambayo mtoto atazaliwa. Mtoto anaweza kuzaliwa siku chache baada au hata wiki kadhaa baada ya siku ya makadirio. Kwa kawaida mtoto anaweza kuzaliwa siku yoyote katika wiki ya 37 hadi wiki ya 43.
- Hata mashine maalum za ultrasound huwa zinafanya tu makadirio na haiwezi kukupa siku kamili ya kuzaliwa kwa mtoto.
Madaktari wanawezaa
kuweka pressure kwa mama kuwa mtoto lazima azaliwe sasa. Na wanaweza kukupa
sababu kuwa placenta inaweza kuacha kufanya kazi na mtoto kuzaliwa na madhara
au hata kufariki. Lakini kutokana na research iliyofanyika risk ya hii kutokea
ni ndogo sana.
Mara nyingi kuna risk zaidi kutokea kama daktari ataingilia
kazi ya mwili na kuulazimisha kuzaa kabla haujawa tayari. Kama mama hana elimu
yoyote kuhusiana na uzazi au hata kama ana elimu lakini hana confidence, support, msimamo na dhamira, na basi kukubali tu yale anayoambiwa na watu, ni rahisi
sana kukubali kupewa madawa ya kuanzisha uchungu.
Hizi dawa mara nyingi
zitaanzisha uchungu lakini kama mwili hauko tayari basi kutanuka kwa uzazi
kutachukua muda na hapo ndio maumivu yatakapozidi kuwa makali na mtoto mara
nyingi anakuwa affected na haya madawa basi hapo ndio daktari atabidi ashauri
kufanyiwa operesheni. Lakini ukweli ni kwamba hii yote haiko necessary.
Sababu nyingine
ni pale ambapo labor imeanza lakini inachukua kipindi kirefu. Mara nyingi watu
hawafahamu kuwa labour inaweza kuendelea zaidi ya masaa 24 kutokana na mtu na
mtu.
Kwenye
filamu mara nyingi wanaonyesha mtu kashikwa na uchungu maji yamemwagika, kazaa
hapo hapo kabla hajafika hospitali. Lakini katika maisha ya kawaida ni nadra
sana kutokea. Hasa hasa kwa mtoto wa kwanza. Wanasema kuwa avg ni masaa 12 hadi
17 lakini kuna wanawake ambao wanakuwa kwenye labor siku 3 hadi 4 yaani masaa
72 hadi 96 kuna wale ambao wanabahatika na inakuwa fupi masaa mawili hadi
matano hivyo inategemea.
Mara nyingi
wale wenye labour ndefu huwa maumivu yanaanza na kutulia na pia njia inachukua
muda kufunguka. Kwa wale wenye labor fupi itachukuwa muda mfupi na maumivu
yatakuwa makali sana kwa vile njia itapanuka kwa muda mfupi.
Ila
kwasababu watu wengi siku hizi hatuna subira
na wauguzi wanashughuli nyingi hawawezi kukaa kukusubiria wewe
tu mpaka uzae hivyo mara nyingi ikipita baada ya masaa fulani wataanza kukupa
ushauri wa kukupa dawa ya kuongeza spidi ya labor hii dawa ndiyo itaongeza
spidi lakini ndio maumivu yatazidi na kuwa makali kupita kiasi kwasababu yale maumivu ni ya dawa na sio
maumivu asilia hapo ndio mara nyingi mwanamke atashindwa kuvumilia na kukubali
operesheni.
Kwa wale
ambao labor itachukua muda mrefu inahitajika stamina ya hali ya juu ikiwa
pamoja na mwili kuwa fit kwa mazoezi, lishe bora na maji ya kutosha ili kuendelea
kuwa na nguvu kwa kipindi chote hichi. Hapa kama huna stamina ndio hapo kuna
uwezekano mkubwa wa kukubali madawa na hatimaye operesheni.
Kama
mwanamke anafahamu haya na kajitayarisha vya kutosha unaweza kuendelea na labor
nyumbani mpaka ikifikia stage fulani ya labor. Tutaongelea kwa undani ni stage gani na dalili gani wiki
zijazo.
Tatizo lingine ni position mbali mbali za kuzaa na kumsukuma
mtoto. Kuna position ambazo ukikaa wakati wa labor zinasaidia kutanuka kwa njia
ya uzazi kwa urahisi zaidi. Lakini mara nyingi hospitalini huwa unaruhusiwa
kufanya position moja tu ya kulalia mgongo huku miguu imetanuliwa wakati hii ni
position ngumu sana kwa mama kusukuma na njia ya uzazi kutanuka. Pia watu wengi
hawafahamu hizi position za kuzaa kwa sababu ya kukosa mafunzo.
Sio kwamba
madaktari hawana ujuzi, ila mafunzo yao huegemea zaidi kwa kutumia njia
za kisasa kuokoa maisha ya mwanadamu. Pia mara nyingi wana majukumu mengi na
kuelemewa na kazi. Hivyo ni responsibility yetu sisi kufahamu mambo gani
yanahitaji daktari kuingilia au la.
Sijui kama hili linaendelea kwa tanzania
lakini kwa nchi nyingine ulimwenguni hasa kama marekani mara nyingi hospitali
na daktari watalipwa zaidi kama mama atashauriwa kuzaa kwa operesheni au c-section,
hivyo imekuwa kama biashara fulani. Inasikitisha lakini ndio ukweli wa maisha.
Ndio maana kipindi cha zamani wanawake walikuwa wanazalishwa
na mkunga (midwife) wanawake wazee katika jamii wenye uzoefu wa kutosha, ujuzi
na subira katika shughuli nzima ya uzazi. Hawa wakunga walikuwa na ujuzi wa kiasilia ya jinsi ya kupambana na matatizo mbali mbali na hasa kumsaidia mwanamke mjamzito kupanua njia yake kwa njia hizi. Lakini tumepoteza hizi mila na tamaduni mbali mbali.
4. Maumivu kuonekana kama ni kitu kibaya
Nikirudi katika mambo ya mtazamo wa jamii, maumivu ya uzazi
yanaangaliwa kama ni maumivu makali kuliko yote kwa mwanamke. Ndio maumivu ni
makali lakini jamii haimfundishi mwanamke njia mbali mbali asilia za
kukabiliana na maumivu haya. Pia kama mwanamke hana mafunzo, confidence,
dhamira na support ya kutosha hataweza kuyastahimili maumivu haya.
Hivyo pale
asikiapo tu maumivu makali na daktari akisema anaweza kumpa kitu kupunguza
maumivu wengi wetu hukimbilia kukubali wengine huomba wenyewe hata bila kupewa.
Kitu ambacho hatufahamu ni kwamba madawa haya
mbali na kupunguza maumivu yanauwezo wa kuleta effects nyingine kwa mama
mjamzito na mtoto ambazo husababisha daktari kulazimika kufanya operesheni.
Madhumuni
ya maumivu ya uzazi ni kumsukuma mtoto chini na kutanua njia ya uzazi. Hivyo
tukiingilia hii kazi kwa kutumia kemikali ndio pale kuzaa kunaweza kuishia kuwa
kwa operesheni.
5.Mafunzo, elimu na support pamoja na Mtazamo mbaya kuhusiana na mimba na kuzaa katika jamii
Kwa sababu hamna mafunzo maalumu ya uzazi ya kuaminika kutoka
kwa mama zetu au mkunga mwenye ujuzi na mambo ya uzazi na hata jamii kwa ujumla.
Ninaamini tunafundwa mengi kuhusiana na utunzaji wa nyumba
na waume wetu katika ndoa au hata kuwa na boyfriend kutoka katika jamii kwa ujumla.
Lakini likija katika jambo la kuzaa na uzazi ni kama vile wazungu wanasema ”taboo”.
Ni nadra sana kusikia wanawake wanapeana masomo kuhusu uzazi na ukisikia
wanaongelea haya mara nyingi wanapoteshana kwa vile wale wanaowahadithia wenzao
pia hawana ujuzi au utaalamu unaotosha. Mara nyingi story zinazoongelewa ni za
kutishana tu.
Ili mwanamke mjamzito aweze kuzaa kwa njia natural anabidi
kwanza apate mafunzo ya kutosha kuhusiana na mwili wake kwa kipindi hiki ili
afahamu jinsi ya kujitunza na pia ili afahamu kama kuna tatizo au la.
Pia anabidi apate support ya hali ya juu
kutoka kwa jamii inayomzunguka na wale watu karibu kwake ili aweze kuwa na
confidence ya kukabiliana na uzazi. Mara nyingi kwasababu wanawake wengi
hatujui kitu chochote kuhusiana na kuzaa au labor kwa ujumla tunakuwa kama
victims tunasubiri tu siku ifike tuende hospital madaktari na manesi wafanye
kila kitu.
Ila tukiwa na elimu ya kutosha kuna vitu ambavyo tunaweza kufanya
kurahisisha zoezi zima la kuzaa ikiwa ni pamoja na njia natural za kufungua
uzazi, jinsi ya kutambua dalili mbali mbali za labor kuanza, ni vitu gani
vitatokea na ni vya kawaida, ni vitu gani ni hatari na jinsi ya kukabiliana na
mambo haya.
Pia kwa sababu ya uoga na kutokufahamu
wanawake wengi wanapanga tu kufanya operesheni
kwa vile hawafahamu kuna njia natural za kupambana na mumivu ya labor na madhara ya dawa mbali mbali ambazo zinaweza kutolewa wakati wa kuzaa.
Pia support katika familia ni kitu muhimu sana kama hamna mtu katika familia yako anafahamu
chochote kuhusiana na hili. Basi inamwia vigumu mwanamke kukabiliana na mambo
mbali mbali yatakayotokea na kufanya maamuzi ya busara.
Support kutoka kwa familia na elimu au mafunzo pia itamsaidia mwanamke kuweza kuchagua wauguzi wazuri zaidi ambao watakubaliana na maombi yake na kumsikiliza.
Jamii nayo kuzidisha woga kwa mwanamke:
Kila kukicha huwa tunasikia story jinsi mwanamke mwingine alivyopata
experience mbaya wakati wa uzazi. Ukimuuliza
mwanamke yoyote yule ambaye hajaza au hata yule ambaye amezaa lakini hakuwa na
experience nzuri kuwa kwanini wanaogopa kuzaa watakuambia wanaogopa mambo
yafuatayo.
Maumivu makali ya uzazi na kuogopa labda kitu kibaya
kitatokea.
Wengi wanaogopa vitu kama kukatwa huko chini wakati wa uzazi ili
kuongeza njia.
Wanaogopa kuchanika wakati wa kusukuma mtoto.
Wanaogopa uke kutanuka
na kutorudi katika hali ya kawaida na kuharibu raha au kusikia maumivu wakati
wa tendo la ndoa.
Wanaogopa mtoto kupatwa na tatizo au kufariki au hata mama
kupatwa na tatizo wakati wa kuzaa.
Wanaogopa kujiachia haja kubwa wakati wa
kusukuma mtoto. Wengine wanaogopa kuzaa kwa operesheni.
Kwa kweli kuzaa si kazi lelemama na nasema hivi sio kwa
kutisha ila tuichukue kama changamoto ya kwamba tujifunze jinsi ya kukabiliana na siku
hiyo muhimu ili mwili uweze kufanya kazi yake kisahihi.
Katika wiki zijazo nitaongelea kiundani kila stage ya labor
na mambo gani mwanamke anaweza kufanya kusaidia labor. Na vitu gani vikitokea
ajue ya kwamba ni vya kawaida na vita pita na awe na subira au vitu gani ni
muhimu kwa daktari kuingilia ili kuokoa maisha ya mama na mtoto. Na jinsi dawa fulani zinavyoaffect mwili wa mama na mtoto. Ni wakati gani operesheni ni muhimu kwa mama mjamzito n.k
Katika swala hili zima la elimu kwa mwanamke mjamzito
ningependa kushauri wanawake wote pale wanapogundua kuwa wana ujauzito au
wanataka kupata ujauzito basi washauriane na baba wa mtoto au mtu wa karibu
kwako kupata mafunzo maalumu ya uzazi. (birth classes)
Mchukue muda msome mambo kuhusiana na
uzazi kwenye tovuti mbali mbali hasa hasa mambo kuhusiana na kuzaa kwa njia ya
kawaida. Vitu kama ni mambo gani yatatokea wakati wa kuzaa na jinsi ya
kukabiliana nayo.
Kuna website nyingi sana online kutoka kwa wanawake ambao
wamezaa kwa njia ya kawaida na wana experience nzuri.(nadhani hapo mbele ninaweza kutoa links za tovuti nzuri kwa hili kama kuna watu wangependa kuzifahamu) Ukisoma story hizi na
kuangalia video mbali mbali fupi zinazonyesha story zao, utapata faraja hata confidence kuwa
inawezekana kuzaa kwa kawaida.
Hii itaondoa woga na wasi wasi ambao ni
mojawapo cha chanzo cha matatizo katika kujifungua. Wakati mwingine zoezi zima la kuongezeka kwa njia la uzazi linaweza kusita kama mwili uko stessed, na umejawa na woga au anxiety.
Pia msome jinsi ya kujitayarisha
iwapo tatizo lolote litatokea na mnaweza kufanya kitu gani au kukabiliana vipi
na matatizo haya.
Samahani kwa kuwachosha na jibu refu lakini nataraji nimewafumbua macho katika hili. Kwa yale niliyoyaongelea kijuu juu nitayaongelea tena kiundani wiki zijazo
God knows what any female bears [in her womb], and by how much the wombs
may fall short [in gestation], and by how much they may increase [the average
period]: for with Him everything is [created] in accordance with its scope and
purpose. [Qur'an 13:8]
It has been of help.
ReplyDeleteThanks
Asante sana lakini dalili za mimba ya kwanza za uchungu ni zipi naomba unisaidie
ReplyDelete