Yeast infection ni aina ya fungus inayokua
kwenye sehemu ya uke.
Wakati wa ujauzito kwa ajil ya mabadiliko mbali mbali ya
kikemikali na hormone basi mwili unashindwa kuregulate hali ya eneo hili. Kwa
vile kuna sukari nyingi zaidi katika eneo hili ambao hao fungus wanatumia kama
chakula huongeza kuzaliana kwa vijidudu hivyo.
Pia wakati wa ujauzito kwa ajili ya kuongezeka kwa damu mwilini. Figo linafanya kazi ya ziada kusafisha damu hivyo sehemu hii inakuwa na uwezekano wa kupata maambukizi na infection katika wakati huu.
Mara nyingi wanawake wajawazito wanapata yeast
infection kwenye trimester ya pili ya ujauzito (kuanzia miezi minne had sita ya
ujauzito).
Hii hutokea pale ambapo acid na yeast ambayo
hukaa katika eneo la uke haziko balanced hivyo kusababisha kukua kwa yeast
kwenye eneo hili.
Yease Infection mara nyingi husababishwa na:
Mabadiliko ya hormone yanayosababishwa na
ujauzito au kabla ya kupata damu ya mwenzi( kwa wale ambao si wajawazito)
Pia inaweza kusababishwa na kunywa madawa yenye
hormone, antibiotics, steroids, dawa za uzazi wa mpango na madawa ya kusafisha uke.
Kwa wale wenye ugonjwa wa diabetes(kisukari) wanaweza kusumbuliwa na hali hii.
Dalili ya Yeast Infection
Kutokwa na chembe chembe nyeupe, kijani au
njano ukeni ambazo zina harufu ya fungus au yeast.
Kuwashwa na uekundu
katika sehemu hiyo ya mwili
Kusikia kuungua
wakati wa haja ndogo au kujaamiana
Kama una hili tatizo
kutana na daktari ili upate dawa ya kupaka itakayo saidia. Mara nyingi huchukua
siku 10 hadi 14 kupona.
Wakati mwingine mama
anaweza kumuambukiza mtoto anapozaliwa na hivyo kuwa na yeast infection midomoni(thrush).
Jinsi ya kuzuia au kupunguza yeast infection
Fanya zoezi la Tailor Sitting.
Vaa chupi na nguo zenye kupitisha hewa kama vitambaa vya
cotton au usivae kabisa.
Baada ya kuoga unaweza kutumia blow dryer wenye moto mdogo
kukausha sehemu hii.
Baada ya kuogelea oga mara moja. Usibaki au kuvaa nguo
ambazo zimelowa au hazijakauka vizuri.
Usitumie dawa za kusafisha uke au toilet paper na taulo za kike zenye manukato.
Usile vyakula vyenye sukari kwani hivi huongeza ukuaji wa
yeast.
Pumzika ili mwili upate muda wa kupambana na vijidudu au
infections.
Kula mtindi ili kuzuia yeast infection hasa kama unakunywa
dawa za antibiotics.
Kunywa maji mengi na hakikisha hubani mkojo kwani kuweka mkojo kwenye eneo hili kutasababisha wazaliane zaidi.
Osha mikono kabla na baada ya kujisaidia.
Kunywa juice aina ya cranberry itasaidia kuponya kama ndio ugonjwa ndio kwanza umeanza. Hakiskisha haina sukari aina yoyote. Ili ifanye kazi vizuri hakikisha unakunywa 8 ounce glass kila baada ya saa moja kwa masaa 10 na uanze mara moja pale unapodhani una dalili za infection. Jaribu kupata natural cranberry juice ambayo haijatiwa sukari yoyote au kama una matunda yake ni vizuri kuitengeneza mwenyewe.
Kunywa chai ya nettle kila week katika miezi ya mwisho wa ujauzito kutasaidia pia kuongeza nguvu ya figo na kulinda sehemu hii na infection mbali mbali.
Kumbuka kuwataarifu wauguzi na madaktari wako.
No comments:
Post a Comment