Mara nyingi
tatizo la kuchoka wakati wa ujauzito ni la kawaida sana. Hii ni kwasababu mwili wa mama hufanya kazi ya ziada katika kumjenga na kumtosheleza mtoto anayekua
pamoja na mwili wa mama mwenyewe. Mambo mengine yanayochangia ni kubadilika kwa
hormone pamoja na mabadiliko katika hisia na mood za mwanamke.
Lakini pia
kuna uwezekano kuwa mama mwenye hili tatizo akawa anatatizo la anaemia, hanywi
maji ya kutosha au hana maji ya kutosha mwilini(dehydration).
Kama mama
mjamzito na unajisikia uchovu sana kila siku au siku nzima kwa ujumla basi zingatia:
- Sikiliza mwili wako na upumzike pale unapoanza kusikika uchovu.
- Jaribu kupumzika zaidi; yaani tenga muda zaidi wa kupumzika
- Punguza stress katika maisha yako na jaribu kupata usingizi wa mchana
- Punguza masaa unayofanya kazi
- Usifanye mambo mengi au kazi nyingi kwa wakati mmoja au mpaka uelemewe punguza kazi zako za kila siku
- Hakikisha unapata diet nzuri ambayo iko balanced special kwa mama mjamzito
- Kunywa maji mengi ya kutosha na matunda ili kuongeza maji mwilini
- Hakikisha unafanya mazoezi ya kutosha hasa hasa yale ya relaxation.
- Mwili wako unahitaji protein ya kutosha kwa kipindi hiki, ukosekaji wa protein utasababisha utamani vitu vitamu vitamu vyenye sukari. Kula vyakula vyenye sukari au asali havishauriwi maana utasababisha mbadiliko wa mood, depression pamoja na kuchoka. Ni bora kama unasikia njaa ule vitafunio vingi kila baada ya masaa kadhaa vyenye jamii ya karanga, jibni, mtindi na samaki wadogo kama dagaa.
Chai ya Raspberry |
Chupa ya Peppermint |
Chupa ya Spearmint |
No comments:
Post a Comment