Wednesday, April 18, 2012

Tatizo la kukosa au kushindwa kwenda chooni (Constipation) kwa mama mjamzito


Wakati wa ujauzito kuna mabadiliko yanayotokea kwenye mwili yanayosababisha kupungua kwa kazi inayofanywa na utumbo wa kusafirisha masalio ya chakula. Hii hali inasababisha mwanamke mjazito kushindwa kwenda haja kubwa mara kwa mara au kiurahisi.

Stress katika hisia za mwanamke(emotional stress), mabadiliko ya diet ya chakula paloma na ratiba ya kulala na usingizi pia inachangia hali hii.

Wanawake wanaokunywa dawa ya virutubisho vya Iron vyenye Ferrous Sulfate pia zinaweza kusababisha hali hii. 

vidonge vya Iron Ferrous Sulfate ambavyo baadhi ya wamama wajawazito hutumia


Hivyo mama ajitahidi kupata mahitaji yake ya Iron kutoka kwenye  vyakula maalum vyenye Iron au kwenye mitishamba kama mzizi wa "Yellow Dock"

Mzizi wa mmea wa Yellow Dock una Iron nyingi na kirutubisho kizuri asilia kwa mama mjamzito anayehitaji Iron

Kama huwezi kupata mmea wenyewe unaweza ukaenda kwenye maduka yanayouza vyakula au mitishamba ya asilia ukapata ambayo tayari yameshatengenezwa kama chai au maji yake.
Maji ya mmea wa Yellow Dock


Kama unahili tatizo:
  • Usile vyakula au vitafunio vilivyotengenezwa kwa unga wa ngano mweupe mfano kama mkate, biscuti, pizza, chapati,aina zozote za keki, macaroni na spaghetti, donuts, bagels, pancakes.Badala yake kula vyakula vilivyotengenezwa kwa unga wa whole grain kama vile wali wa brown(brown rice), tortillas, oatmeal, bran muffins, whole wheat bread(brown bread). 
Mfano wa vyakula vilivyotengenezwa na Whole Wheat
Mifano zaidi ya vyakula vyenye Whole Wheat


  • Kula matunda mengi fresh au yaliyokaushwa jaribu kuchanganya aina ya matunda unayokula.
  • Kunywa maji mengi na ongeza maji mwilini kwa kunywa soup, maji ya matunda na mboga fresh, na herbal chai.
  • Punguza nyama aina za sausage, ham, bacon na red meat
Nyama Ya Ham


Nyama ya bacon
Sausage
Nyama ya Pastrami
Mifano mbali mbali ya nyama aina ya red meat

  • Fanya mazoezi maalum kwa mama mjamzito kila siku.
  • Weka kiti kidogo au stool chini ya miguu wakati unaenda chooni
    Usitumie madawa ya kusaidia kulainisha chakula pia jaribu kurelax wakati wa kwenda chooni.
  • Hakikisha hubani haja kwa muda mrefu pale utakapokuwa mbali na choo au shughuli nyingi. Jaribu kutenga muda wa kwenda chooni.
  • Juice ya matunda ya prune au kula haya matunda kutasaida kulainisha utumbo na kurahisisha haja. 

Tunda la Prune



  • Pia mimea ya Rhubarb, figs na maple syrup inasaidia kulainisha tumbo. Kula mboga za majani kwa wingi. 

Mmea wa Rhubarb



Tunda aina ya Figs

Maple Syrup




  • Ngano ya Amaranth, mmea wa Lamb's quarter na majani ya violet haya yote ni mazuri kwa tumbo. Unaweza kuyachemsha halafu kunywa maji yake. Kutasaidia kurahisisha tumbo la haja.
Amaranth
Mmea wa Lamb's Quarter



Mmea wa Violet na majani yake


No comments:

Post a Comment