Monday, April 16, 2012

Tatizo la Hemorrhoids/Bawasiri kwa mama mjamzito

Tatizo la Hemorrhoids/Bawasiri limefanana na tatizo tulilokwisha ongelea la  vericose veins(kuvimba kwa mishipa ya damu)


Ili kuzuia hili tatizo hakikisha unamzunguko mzuri wa damu kwa kufanya mazoezi maalum ya mama mjamzito. Kwasababu hili tatizo hutokana na pressure kuongezeka kwenye mishipa ya damu ya mama mjamzito.


Hemorrhoids au Baswiri

Mama mjamzito anabidi ajitahidi kutokustress mwili kwa kutokusimama kwa kipindi mrefu. Kuongezeka kwa msukumo wa damu wakati wa ujauzito unaweka stress kwenye mishipa, hii pamoja na kuongezeka kwa hormone aina ya Progesterone inalegeza misuli ambayo inaweza kusababisha kuvunjika kwa mishipa. Hata kama hukupata hili tatizo wakati wa ujauzito upo uwezekano wa kupata hemorrhoids au vericose veins baada ya kujifungua.

  • Kunywa maji mengi ili kuzuia tatizo la constipation au kutoweza kwenda haja kubwa.
  • Fanya zoezi la Pelvic rocking
  • Weka miguu juu ya kiti wakat unaenda haja kubwa.
  • Fanya zoezi la kegels
  • Kunywa maji na matunda kwa wingi
  • Oga maji ya uvuguvugu yenye mitishamba ya kusaidia kuponya hemorrhoids.

Jinsi ya kujiponya na maumivu ya hemorrhoids.

Chukua baking soda kiasi ya moto au baridi kisha paka kwenye sehemu yenye hemorrhoid hii itasaidia kupunguza maumivu ya kuwashwa (wakati wakupaka utasikia joto kidogo au kama kuungua kidogo katika sehemu hiyo)

Unaweza kutumia maji ya ndimu au herb aina ya  ”Witch Hazel” kuzuia maumivu kuvimba na utokaji wa damu hii itauma kidogo.

Unaweza kusaga vizi halafu paka kwenye sehemu kupunguza uvimbe na maumivu.

Chukua kitunguu saumu kilichopakwa mafuta halafu weka kwenye gozi gozi maalum au plasta ya vidonda kisha weka kwenye hiyo sehemu yenye hemorrhoid kwa usiku mzima.

Kama tatizo ni zito basi unaweza chukua majani ya ndizi za kupika au herb(mitishamba) aina ya ”witch Hazel” tengeneza vikombe 8 kwa kuchukua 4 oz ya herb(mitishamba) halafu katika nusu gallon ya maji yaliyochemka kisha yaache yakae kwa masaa 8 Chuja mitishamba ili kupata maji yake. Weka kwenye  beseni kisha ukae humo kwa muda wa dakika kumi na tano 15 mara mbili kwa siku. Rudia kwa mara nyingine pale utakapojisikia. Hemorrhoids zote zitapotea baada ya siku chache. Mitishamba mingine inayoweza kutumika ni pamoja na ”Comfrey Roots”, ”White Oak Bark”, ”Sea grape leaves/bark”

No comments:

Post a Comment