Uongezekaji
wa uzito wa mtoto, Uongezekaji wa maziwa na uzito sehemu mbali mbali ya mwili, kubadilika
kwa mwenedo wa mwili, kubadilika kwa mhimili wa mwili, uzito na stress kwenye
mafigo na ugumu wa kuamka na kukaa katika viti na vitanda husababisha mwanamke
kupata maumivu ya mara kwa mara kwenye mgongo katika ujauzitio wake.
Hakuna dawa
ambayo mama anashauriwa kunywa ili kukabiliana na maumivu haya. Hata dawa za kupunguza maumivu
kama aspirin na panadol hazishauriwi.
Badala yake
maumivu ya mgongo yanaweza kuponywa kwa mazoezi, ulaji wa chakula bora na
baadhi ya herbs/mitishamba maalum.
Kuimarisha misuli ya tumbo kwa mazoezi, kukaa na kulala kwenye viti na vitanda vyenye support ya kutosha inaweza ikasaidia sana
kuzuia uzito wa mtoto kuweka pressure kwenye mgongo.
Kufanya
mazoezi mara kwa mara bila kukosa kutasaidia misuli iimarike na kuweka mhimili
wa mwili na balance sawa. Herbs/mitishamba maalaum inasaidia kuimarisha mafigo.
Mazoezi maalum ya kupunguza maumivu ya mgongo:
Zoezi la Paka-Ngombe(Cat/Cow):
Hili zoezi limefanana na zoezi la Pelvic Rocking ambalo tulishaliongelea kwenye maada zilizopita.
Unaweza kufanya hili zoezi kila siku au pale unaposikia
maumivu kwenye mgongo. Kaa kwenye position ya mikono na magoti chini kwenye sakafu.
Vuta pumzi kwa ndani shusha kichwa chini na weka mgongo juu kama paka. Achia
pumzi na weka kichwa juu na acha mabega yarudi chini. Endelea kurudia zoezi
huku ukivuta na kuachia pumzia. Hili zoezi linaweza kufanywa pia ukiwa
umesimama.
Zoezi la Kutwist magoti na kifua(Knee/Chest Twist):
Mara moja kwa siku au pale usikiapo
maumivu lala chali kwenye sakafu na vuta magoti kuelekea kwenye kifua. Nyosha
mikono pembeni. Halafu taratibu elekeza
magoti upande wa kushoto huku kichwa ikielekea kulia kaa hivyo kwa nusu dakika huku
ukirelax halafu badilisha mwelekeo wa magoti kulia na kichwa kushoto. Fanya
hivyo mara moja au mbili.
Maumivu
yakizidi unaweza kwenda kwa mtaalamu wa massage au chiropractor ambaye anaweza
kunyoosha misuli mbali mbali ya mgongo.
Vitu vya kuzingatia:
- Ukilala jaribu kuweka mito ili iweze kutoa support maeneo ya miguu, mgongo na tumbo.
- Usisimame kwa muda mrefu.
- Kula vyakula vyenye calcium kwa wingi.
- Pata Zoezi la kutembea.
- Relax
kwenye maji ya uvuguvugu
-
Fanya mazoezi maalum ya ujauzito la Pelvic Rocking kuimarisha misuli na kusaidia kuunyosha mgongo.
- Ukiwa unataka kuinua kitu kizito au kuinama jaribu kukunja miguu na sio mgongo.
- Vaa viatu ambavyo ni vya flat ambavyo vitasaidia kukupa balance na kutoa support kwa miguu na mgongo vizuri.
-
Kaa vizuri na kutembea kwa kunyoosha mgongo yaani usiegemeze uzito wako sehemu moja.
Vyakula vizuri kwa kuimarisha mgongo.
Vyakula vyenye virutubisho vya calcium na magnesium kama tulivyoongelea kwenye maada zilizopita vinaweza kuzuia au pia kupunguza maumivu ya mgongo. Magnesium inaweza kupatikana kwenye mboga za majani, apples, figs, wheat germ mbegu na jamii za karanga hasa hasa almonds.Tunda aina ya Figs nafaka aina ya Wheat Germ Jamii ya karanga aina ya Almonds Pia kunywa maji ya limao glass sita kwa siku itasaidia kusafisha figo na kupunguza maumivu ya mgongo.Herbs/mitishamba inayosaidia kupunguza maumivu ya mgongo
1.Juice ya wheat grass ni nzuri sana kwa maumivu hasa hasa ya mgongo. Hii juici inavirutubisho ambavyo vinasaidia kuimarisha misuli. Kurelax nerve na kufanya uti wa mgongo uwe flexible.
2. Chai au maji ya Nettle Infusion inasaidia kuimarisha na kusafisha figo.
3. Chai ya Comfrey Infusion
inavirutubisho vya kuzuia maumivu ya mgongo pia ina amino acids ambazo
zitasaidia kuimarisha misuli ya tumbo na afya ya mtoto. Comfrey ina virutubisho vya vitamin A, vitamin C, vitamin B12 na B complex, iron, potassium, zinc, selenium, na copper. Unaweza pia ukapaka mafuta ya Comfrey kwenye mgongo kupunguza maumivu.
Chai ya Comfrey |
Mafuta ya Comfrey |
Njia nyingine za kupunguza maumivu
1. Kuoga maji
ya moto, au weka maji ya moto kwenye chupa halafu iweke sehemu ya mgongo yenye
maumivu, unaweza pia ukajikanda kwa taulo la maji ya moto ili kupata unafuu wa
maumivu.
2. Unaweza
kununa mafuta hususan ya Tiger balm, olbas, zheng gu shui, wintergreen oil. Haya mafuta yakipakwa kwenye mgongo yanaweza kupunguza maumivu, stress na pressure kwenye
mgongo. Paka haya mafuta kabla ya kujikanda na maji ya moto.
Mafuta ya Tiger balm |
Mafuta ya Olbas |
Mafuta ya Wintergreeen |
Mafuta ya Zheng Gu Shui |
3. St John’s/Joans
wort ni herb ambayo husaidia maumivu ya misuli weka drop 15 hadi 25 kwenye
glass ya maji halafu jikande nayo kila baada ya masaa kadhaa. Hii husaidia kulegeza misuli na kupungza maumivu. Kama maumivu ni makali
sana unaweza kuongeza drop 3-5 ya herb aina ya ”skullcap tincture”. Hizi herbs husaidia kwa kujipeneyeza katika misuli na nerve na kuirelax. Baada ya misuli kurelax basi mifupa ya mgongo hujinyoosha.
St John's Wort Herb |
Maji ya Herb ya Skullcap |
No comments:
Post a Comment