Mayai
ya mwanamke ni mojawapo ya viungo ambavyo vimeshatengenezwa kabla hata
mwanamke hajazaliwa, yaani tangia akiwa fetus ndani ya tumbo la mama
yake.
Haya
mayai yanakuwa tayari pale msichana anapopata menstruation yake ya
kwanza average ya miaka 12 hadi 14. Kuanzia hapo hadi pale atakapofikia
menopause/kikomo cha menstruation kwa mwanamke (average miaka 51) mayai
yake na fertility yake hupungua anavyozidi kuzeeka. Yaani katika ujana
wake, teenage na 20s ni muda ambao ni rahisi zaidi kutunga mimba. Na
kuanzia miaka 30 had 51 uwezo huu unapungua kwa kiasi kikubwa mpaka
unapoisha kabisaa.
Wakati
kwa wanaume wao sperm cell zinaanza kutengenezwa pale wanapo
balehe(puberty age) mpaka siku atakayo kufa. Hii inamaanisha kama
mwanaume akiwa katika hali nzuri ya kiafya anaweza kumpa mimba mwanamke
hadi afikapo uzeeni iwapo mwanamke bado hajafikia menopoase na ni
fertile.
Sasa tuangalie ni vitu gani vinaweza kuaffect kwa kiasi kikubwa utungaji wa mimba(fertility).
Wanaume
na wanawake wanaweza kuwa affected na vitu kama kemikali katika
mazingira ya kila siku, diet au lishe na hata matukio mbali mbali katika
maisha kama stress.
Hii inaweza hata kuaffect quality ya mayai au sperm ambayo pia inaweza kumuaffect mtoto.
Basi kama wewe na mwenzi wako mnajitayarisha kupata mimba mnapaswa miezi kadhaa kabla muache vitu vifuatavyo:
- Kunywa dawa mara kwa mara kama si lazima (zikiwemo aspirin na antibiotics)
- Utumiaji wa hali ya juu wa vinywaji vikali, pombe na wine
- Caffeine (kahawa, black tea, cola, chocolate)
- Utumiaji wa sigara
- Hakikisha wote mnakula vyakula ambavyo ni balanced diet.(nitafafanua zaidi maana ya balanced diet katika nakala zijazo)
- Radiation inayoambatana na x-ray na teknologia zingine
- Rangi na dawa za kubadilisha nywele
Hii haimainisha ya kuwa usipoachana na hivi vitu huwezi kupata mimba la hasha. Bali kama wewe tayari una matatizo au unataka chance ya kupata mimba kuongezeka haya mambo yanaweza kusaidia. Na kama ungependa kuwa na mimba yenye afya njema(healthy pregnancy) na mtoto mwenye afya njema basi unabidi uzingatie hivi vitu (hasa hasa kama ungependa kuhakikisha ukuaji mzuri wa ubongo wa mtoto yaani brain development).
Hii pia itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matatizo yanayoweza kutokea wakati wa uzazi.
Kama wewe unamatatizo ya fertility au kupata mimba basi hapo mbeleni tutaongelea vyanzo na njia mbalimbali zinazoweza kusaidia upatikanaji wa mimba.
No comments:
Post a Comment