Monday, June 11, 2012

Stage ya kwanza ya labor


Kuna stage tatu ambazo mwanamke ambaye anajitayarisha kujifungua anapitia wakati wa labor.

Hizi ni:
 • Stage ya kwanza ya Labor (Dalili za kuingia labor na mwanzo wa maumivu na kupanuka kwa njia ya uzazi)
 • Stage ya Mpito/Transition (Kuvuka kwa stage ya kwanza kwenda kwenye stage ya Pili)
 • Stage ya Pili ya Labor (Kusukuma mtoto na Kutoa placenta)

Katika maada ya leo tutaongelea dalili za kuanza kwa labor na ni vitu gani vitatokea katika stage hii ya kwanza.

Kabla ya kuanza kwa labor kuna vitu fulani vitatokea mwilini ili kumtayarisha mama na mtoto kwa labor halisi.

Hivi ni pamoja na kupata
 • Braxton Hicks contractions – huku ni kubana na kuachia kwa misuli ya uterus ili kumsukuma mtoto chini. Tofauti na contractions za kweli za labor hizi huja na kuacha na huwa hazina ratiba maalum. Huwa zinaanza kutokea miezi mitatu ya mwisho wa ujauzito.
 • Kuongezeka kwa damu mwilini.
 • Kutoka kwa hormone za relaxin na hyaluronidase – Hormone hizi husaidia kulegeza misuli ya chini ya tumbo na hips ili kuongeza njia ya uzazi.
 • Kutengenezwa kwa Colostrum – maziwa ya mwanzo yenye virutubisho na kinga maalum kwa ajili ya mtoto atakayezaliwa.
 • Kulainika kwa cervix – cervix ni ufunguo au njia ya uterus. Wakati wa ujauzito njia hii inazibwa na utepe mzito ”mucous plug” ili kuzuia vijidudu kumfikia mtoto na pia kuziba njia ya uzazi wakati wa ukuaji wa mtoto.

 • Kutoka kwa utepe wa mucous plug kwenye cervix – Moja wapo ya dalili za kuanza kwa labor ni kutoka kwa utepe wa mucous plug ukeni. Utepe wa mucous plug unaweza kutoka na damu kidogo.

Jinsi mwili unavyofanya kazi wakati wa Stage ya Kwanza ya Labor

 • Kuanza kwa conractions – Kubana na kuachia kwa misuli ya uterus na kusukumwa kwa mtoto. Misukumo hii huambatana na maumivu makali sehemu ya chini ya tumbo ambayo itaendelea kwa ratiba maalum.
 •  Mama Kusikia njaa.
 •  Mama Kusikia kiuu.
 • Mama anaweza kupatwa na tumbo la kuharisha.
 • Dilation – Kufunguka kwa cervix ikiambatana na kutokwa kwa utepe wa ”mucous plug”. Kufunguka huku hupimwa kwa centimeter kidole kimoja kikiwa kama centimeter moja (1). Cervix itafunguka kwa centimeter moja kwa kila saa ya labor kwa kawaida lakini hutofautiana mwanamke kwa mwanamke. 0 cm mpaka 4 cm hutokea wakati wa stage ya kwanza ya labor. 4 -7 cm hutokea lavor inapochangamka na kuwa ngumu. 7-10 hutokea wakati wa stage ya mwisho wakati mwanamke anajitayarisha kusukuma. Centimeter 10 ni sawa na ukubwa wa kichwa cha mtoto na wakati huu ndio mtoto anakuwa tayari kuzaliwa.
 • Effacement – Kutanuka kwa cervix ili kuongeza njia na upana wa cervix ili kusaidia mtoto kupita. Kabla na wakati wa ujauzito cervix ya mwanamke ni pana na ndefu inchi moja au mbili. Wakati wa stage ya kwanza ya labor cervix itaanza kuwa fupi na kupanuka kitendo kinachoitwa effacement au kuiva kwa cervix. Inaweza kuchukua wiki kadhaa mpaka cervix kufunguka kabisa. Effacement hupimwa kwa asilimia. 0% maana yake effacement bado haijatokea na cervix bado haijafunguka. 50% maana yake effacement imefunguka nusu. 100% maana yake cervic imefunguka kabisa.
 • Kama ni mtoto wa kwanza kwa mama, kitendo kitakachotokea kwanza ni effacement ikifuatiwa na dilation. Kama mama kashazaa basi itaanza na kitendo cha dilation kufuatiwa na effacement.
 • Station – Hii ni jinsi gani mtoto ameshuka kwenye njia ya uzazi. Kama mtoto yuko juu ya mifupa basi ni mwanzo wa labor mtoto akishuka chini ya mifupa basi ni karibu na wakati wa kuzaliwa. Hii hupimwa kuanzia -3 , 0 , 3. Ikiwa  -3 kuonyesha kuwa mtoto yupo juu na 3 kuonyesha kuwa mtoto kashuka chini.
 
    
 •  Kutokwa kwa damu – hii ni mojawapo ya dalili ya kuwa cervix inafunguka na kuwa ni mwanzo wa labor. Damu hii itakuwa rangi ya pink au brown.
Kwa wakati huu mama hashauriwi kulalia mgongo kwani kulalia mgongo kutasababisha uterus kushuka mbele wakati wa contractions na kufanya maumivu yawe makali zaidi.

Tumeongelea dalili za kuanza kwa stage ya kwanza ya labor sasa tutaongelea jinsi mwili unavyofanya kazi wakati wa stage ya kwanza na kujitayarisha kuingia stage ya pili.

 • Msukumo wa contraction kuwa na nguvu na maumivu makali zaidi.
 • Kuendelea kuwa na kiuu.
 • Kuondokewa kwa aibu.
 • Kupungukiwa kwa hamu ya kula.
 • Kutaka kwenda haja ndogo mara kwa mara.
 • Kuendelea kwa dilation na effacement.
Kuna uwezekano wa contractions kundelea lakini kufunguka kwa cervix(dilation kusimama) hii husababishwa na:
 • Maumbile
 • Kulainika kwa misuli na mifupa
 • Kuongezeka kwa hormone mwilini
 • Kutengenezwa kwa kinga kwa ajili ya mtoto
 • Baadhi ya misuli ya mwili kupumzishwa
 • Kila mwanamke yuko tofauti kwa hiyo masaa ya kuwa katika stage hii ya labor hutofautiana.Hivyo mama asife moyo kama labor itasimama kwa muda.


Dalili nyingine ya kuwa mama ameingia katika stage ya mwanzo wa stage ya kwanza ya labor:
 • Mwanamke anaweza kuwa na furaha ya kuwa siku imefika lakini kutokuwa na uhakika kama labor imeanza kiukweli ukweli.
 • Mwanamke kutoweza kutulia sehemu moja, kutembea tembea, kuongea sana, kufanya shughuli kama kusafisha nyumba.
 •  Contractions zitapishana kwa dakika 10 au chini ya dakika 10 na kuendelea kwa sekunde 45 -60 na kuongezeka kwa nguvu na kukaribiana zaidi.
 • Contractions kuwa na maumivu makali sana ifikapo sekunde ya 30. Kusikia pressure na maumivu kwenye sehemu ya chini ya tumbo. Kutembea na kuwa busy kutasaidia kwa wakati huu. Mwanamke anaweza kuona mabadiliko mengi kwenye mwili wake kwa wakati huu.
 • Mwanamke ajitahidi kula kunywa maji na kupumzika iwezekanapo ili kutunza nguvu atakayoihitaji hapo baadaye.
 • Kutembea kutasaidia kufungua njia ya uzazi. Kama labor ikisimama usivunjike moyo. Endelea kupata chakula na kupumzika hiki ni kitu cha kawaida.
 Dalili za kuwa mwanamke sasa yuko katika stage ya kwanza ya labor. 
 • Mwanamke kugundua kuwa labor inaanza haswa, kuwa na moyo kuwa anauwezo wa kukabiliana na yale yaliyo mbele yake.
 • Atajaribu position mbali mbali kuona ipi yuko comfortable zaidi wakati wa maumivu.
 • Kutembea kwa wakati huu ni muhimu sana.
 • Maumivu yamekuwa makali zaidi lakini mwanamke atapendelea kuendelea na kazi wakati wa kutulia kwa contractions.
 • Anaweza kuwa na njaa kutokana na labor imekuwa ikiendelea kwa muda gani.
 • Anaweza kuendelea kuongea au kufanya shughuli wakati wa maumivu lakini inaanza kuwa vigumu zaidi.
 • Mabadiliko ya mwili yanaanza kuwa ya kawaida.
 • Contractions zinaendelea kuwa zenye nguvu na nyingi zaidi. Zitapishana kwa muda wa dakika tano na kuwepo kwa sekunde 60.
 • Kuongezeka kwa pressure kwenye sehemu ya chini ya tumbo na kufunguka kwa sehemu hiyo. Kupatwa na maumivu ya mgongo. Kusikia maumivu kama ya siku za mwezi kwenye tumbo.
 • Kusikia kutanuka kwa eneo la chini ya tumbo.
 • Zoezi la pelvic rocks litasaidia kupunguza maumivu kwa wakati huu.(tulishaongelea jinsi ya kufanya hili zoezi kwenye maada zilizopita)
 • Kwa wakati huu anahitaji kutiwa moyo na upendo kutoka kwa watu karibu kwake.
 • Anahitaji nafasi na upepo na aendelee kutembea.
 • Endelea kuhesabu contractions kuona zinaendelea vipi.
 • Jaribu kutotumia nguvu zako kwa kipindi hiki maana ni vigumu kujua utakuwa kwenye labor kwa kipindi gani. Jaribu kuwa busy au fanya kitu cha kufurahisha ili muda uende kwa kasi.
Dalili za kuishia kwa stage ya kwanza ya labor.
 •  Mwanamke kuanza kuingiwa na uoga pale maumivu na contractions zinapozidi.
 •  Mwanamke kutotaka kusumbuliwa na kuwa serious zaidi.
 •  Kuondokewa na aibu
 •  Aendelee kutembea lakini atembee kwa taratibu zaidi.
 •  Anaweza kutaka kupumzika.
 •  Kufumba macho na kusikilizia maumivu.
 • Anaweza kupenda kukaa kwenye choo.
 • Njaa kuondoka.
 • Kutotaka kuongea tena.
 • Kutokwa na jasho .
 • Kutokwa kwa maji ya uzazi.
 • Contractions kuwa kali zaidi kutokuwa na muda wa kupumzika au kupishana kwa maumivu haya. Kuendelea kwa sekunde 60 au zaidi. Kuweka pressure kwenye mfuko wa mkojo na kutaka kwenda haja mara kwa mara.
 • Kazi inakuwa ngumu zaidi, Maumivu makali zaidi mwanamke ajaribu kuwa relaxed kwa kipindi hiki. Kwa sababu kuwa na wasi wasi au uoga kwa wakati huu kutazidisha maumivu zaidi. Pressure kuwa kali zaidi kwenye sehemu ya chini ya tumbo.
 • Ikiwezekana mama akae kwenye sehemu yenye giza au kuzimwa kwa taa
 •  Mama aendelee kutembea tembea na kutokulala au kukaa sehemu moja.
 • Watu wasiweke pressure kwa mama kwa wakati huu
 • Ajitahidi kunywa maji na kwenda chooni mara kwa mara
 • Mama aendelee kuwa na subira katika kipindi hiki na kujaribu kurelax kwasababu labor hutofautiana na huweza kuchukua muda mrefu au kuwa fupi.
 Kama huna uhakika kama labor imeanza au la ni vizuri:
 • Kupumzika au pata usingizi
 • Kunywa maji ya kutosha
 • Kutembea
 • Kuoga

Dalili ya kuwa labor yako inaenda pole pole
 • Contractions zinaanza na kusimama
 • Contractions zinapishana kwa dakika 10 hadi 20
 • Contractions hazikaribiani
 • Contractions hazichukui muda mrefu
 • Contractions haziongezeki kwa ukali au maumivu

Dalili ya kuwa labor yako inaendelea kwa mwendo wa kawaida
 • Contractions zinaenda kwa mwendo wa kawaida
 • Contractions zinapishana kwa chini ya dakika 10 au dakika 10
 • Contractions zinaendelea kwa sekunde 60
 • Contractions zinakaribiana, zinakaa kwa muda mrefu zaidi na zinakuwa kali zaidi jinsi saa zinavyoenda
Dalili ya kuwa labor yako itakuwa fupi sana
 • Contractions zinaanza kwa kukaribiana
 • Contractions zinaanza kwa kuchuku muda mrefu au kuwa ndefu
 • Contractions zinakuwa kali sana
 • Dalili zako zinaanza moja kwa moja bila stage ya mwanzo ya kwanza ya labor.


Mara nyingi wauguzi watafanya uchunguzi kuona jinsi labor inaendelea. Katika uchunguzi huu watatumia mikono au vidole kupima  dilation, effacement, station na jinsi mtoto alivyokaa tumboni.

Kama ikiwezekana ni vizuri kuepukana na vipimo hivi kwasababu vinaweza kusababisha kuchanika kwa mfuko wa uzazi kabla ya muda wake(premature rapture of membranes), kusababisha infection na vijidudu kuingia kwa mtoto, vipimo hivi vitampa mama maumivu ya zaidi, wakati mwingine vipimo hivi si sahihi, na huweza kuongeza risk ya kufanyiwa operesheni.

Kama maji ya uzazi yameshamwagika si vizuri kufanyiwa vipimo hivi.

Katika maada zijazo nitaendelea kuongelea stage ya pili ya labor na position mbali mbali za kusukuma, dawa mbali mbali zinazoweza kutumiwa wakati wa labor na madhara yake, Vitu gani vinaweza kutokea ambavyo vinahitaji umakini zaidi na kuweza kusababisha operesheni,vitu gani vitatokea wakati wa operesheni, ni vitu gani natural mama anaweza kufanya kwa wakati huu aidha kuharakisha labor au kuanzisha labor iwapo inachelewa, kazi ya baba au watu wa karibu kwa mama wakati wa labor.

No comments:

Post a Comment